Pata taarifa kuu

Mkuu wa Umoja wa Mataifa aonya kuhusu 'kurudi nyuma' kwa haki za wanawake

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameonya siku ya Ijumaa Machi 8 dhidi ya "hatua ya kurudi nyuma" kwa haki za wanawake, katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea, wakati wa siku ya kimataifa ya Machi 8.

Wanawake wa Peru waandamana kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Mei 8, 2018.
Wanawake wa Peru waandamana kusheherekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake, Mei 8, 2018. Luka GONZALES / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Duniani kote, kuna tishio la kurudi nyuma kwa haki za wanawake, na wakati mwingine kurudi nyuma kwa maendeleo yaliyopatikana katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea," katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameonya wakati wa Siku ya Kimataifa ya Wanawake katika makao makuu ya shirikahilo mjini New York.

Kwa zaidi ya karne moja, watu kote ulimwenguni wameadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake mnamo Machi 8.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake (IWD) ilikua kutokana na harakati za wafanyakazi.

Mbegu hizo zilipandwa mwaka wa 1908, wakati wanawake 15,000 walipoandamana katika jiji la New York wakidai muda mfupi wa kufanya kazi, malipo bora na haki ya kupiga kura.

Wazo la kulifanya kuwa tukio la kimataifa lilitoka kwa Clara Zetkin, mwanaharakati wa kikomunisti na mtetezi wa haki za wanawake.

Mnamo 1910, aliizungumzia kwenye Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake Wanaofanya Kazi huko Copenhagen.

Pendekezo lake liliungwa mkono kwa kauli moja na wanawake 100 kutoka nchi 17 waliokuwa kwenye mkutano huo.

Siku ya kwanza ya Kimataifa ya Wanawake iliadhimishwa mnamo 1911, huko Austria, Denmark, Ujerumani na Uswisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.