Karibu katika makala wimbi la siasa. Tunaangazia swala la mhubiria Paul Mackenzie Nthenge ambaye aliwashawishi wafuasi wa kanisa lake wafunge bila kula ili wakutane na Mungu katika kijiji cha Shakahola karibu na mji wa Malindi, Pwani ya Kenya.
Nchini Kenya, idadi ya watu wanaohusishwa na imani potofu ya kutokula chakula hadi kufa ili kumwona Mungu, imeongezeka na kufikia 98 baada ya miili mingine kufukuliwa katika kijiji cha Shakahola karibu na mji wa Pwani, Malindi.
Tukio hilo limezua hasira miongoni mwa viongozi, wananchi na wenyeji huku mchungaji anayedaiwa kuwashawishi wauamini wake kufunga mpaka kufa Paul Mackenzie Nthenge akiendelea kuzuiwa.
Kuzungumzia swala hili naungana studioni na Askofu mkuu wa kanisa la anglikana nchini Kenya Jackson Ole Sapit pamoja na afisa wa sheria katika shirika la kutetea haki za binadamu nchini Kenya Haki Afrika Walid Seketi.