Kufutwa kwa kesi zinazowahusu wandani wa rais William Ruto
Imechapishwa:
Cheza - 10:05
Tangu mwaka jana ,idara ya mahakama nchini Kenya imefuta baadhi ya kesi dhidi ya watu walio karibu na rais William Ruto
Mahakama nchini Kenya imefuta kesi nyingi zinazowahusu wandani wake rais William Ruto ,kwa msingi wa kukosa ushahidi.Baadhi ya waliofutiwa mashtaka ni naibu rais Rigathi Gachagua,waziri Aisha Jumwa na Minthika Linturi.
Katika makala haya Eric Theuri ,rais wa chama cha mawakili nchini Kenya ,LSK na Daktari Brian Wanyama mhadhiri katika chuo kikuu cha Kibabii ,Bungoma nchini Kenya ,ambaye pia ni mchambuzi wa siasa ,wanazungumzia hatua hii ambayo imetafsiriwa na wengi kuwa ya kisiasa