Pata taarifa kuu

Ufaransa: Brigitte Giraud atunukiwa tuzo ya Goncourt 2022 kwa kitabu chake "Vivre vite"

Hii ndiyo tuzo ya fasihi iliyotarajiwa zaidi msimu huu. Tuzo ya Goncourt 2022 imetolewa kwa Brigitte Giraud kwa kitabu chake "Vivre vite" (ishi haraka). Uchaguzi ulipunguzwa hadi waandishi wanne.

Brigitte Giraud ashinda Tuzo ya Goncourt 2022 kwa kitabu chake "Vivre vite".
Brigitte Giraud ashinda Tuzo ya Goncourt 2022 kwa kitabu chake "Vivre vite". AFP - JULIEN DE ROSA
Matangazo ya kibiashara

Tuzo la Goncourt 2022 limetolewa kwa Brigitte Giraud kwa kitabu chake "Vivre vite". Kitabu hiki, kilichochapishwa na Flammarion, ni kurejelea kwa matukio yasiyowezekana ambayo yalisababisha kifo cha mumewe. Mwandishi huyo ametiwa moyo na mazingira magumu ya maisha yake, mnamo Juni 22, 1999 huko Lyon, wakati mumewe Claude alipofanya ajali ya pikipiki ambayo haikuwa yake, baada ya kuanguka na kufariki papo hapo. N mwandishi wa kwanza kupokea tuzo hii tangu "Chanson douce" ya Leïla Slimani mnamo 2016, na mwanamke wa kumi na tatu kutunukiwa tangu kuanzishwa kwa Goncourt miaka 120 iliyopita.

Raundi ya kumi na nne

Tamaduni hiyo ni ile ile kwa zaidi ya karne moja: chakula cha mchana katika mgahawa wa Drouant huko Paris, kuamua ni nani aliyeandika riwaya bora zaidi ya Kifaransa ya mwaka. Majaji kumi wa tuzo za kifahari zaidi za fasihi ya Ufaransa, wanaume saba na wanawake watatu, wametoa uamuzi wao.

Mnamo 2022, Brigitte Giraud alishinda katika raundi ya kumi na nne ya kura ngumu sana dhidi ya Giuliano da Empoli, kutokana na sauti ya rais wa jopo la Goncourt, Didier Decoin, ambaye alipewa haki ya kutia tury mbili. Anarithi mikoba ya Msenegali Mohamed Mbougar Sarr. Chuo cha Goncourt kimemchagua mwandishi asiyejulikana sana kwa umma na ambaye hatumii takwimu kubwa za mauzo, hivyo basi kufuatilia ufufuo fulani. Mzaliwa wa Algeria, Brigitte Giraud, anayeishi Lyon (katikati-mashariki mwa Ufaransa), ameandika takriban vitabu kumi, riwaya, insha au hadithi fupi.

Washindi wanne

Uteuzi huo ulikuwa umepunguzwa hadi washindi wanne: waandishi wawili wa Ufaransa, Brigitte Giraud na Cloé Korman, Muitaliano mweye asili ya Uswisi, Giuliano da Empoli, na Mhaiti, Makenzy Orcel.

(pamoja na AFP. Taarifa zaidi zinakujia)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.