Pata taarifa kuu

Mfaransa Annie Ernaux atunukiwa Tuzo ya Nobel ya Fasihi 2022

Annie Ernaux, 82, mwandishi wa Ufaransa, ametunukiwa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka 2022. Ni mwanamke wa kwanza wa Ufaransa kupokea tuzo ya fasihi ya kifahari zaidi duniani. Jina lake lilikuwa likiongelewa kila mahali.

Mwandishi Annie Ernaux, mshindi wa Tuzo la Nobel la Fasihi 2022.
Mwandishi Annie Ernaux, mshindi wa Tuzo la Nobel la Fasihi 2022. © Francesca_Mantovani Editions_Gallimard_
Matangazo ya kibiashara

Chuo Kikuu cha Sweden, kwa mara nyingine, kimekamilisha uchunguzi wake kwa kumtunuku Tuzo ya Nobel ya Fasihi, Alhamisi, Oktoba 6, mwandishi Mfaransa aliyekuwa akitarajiwa sana. Annie Ernaux ni mwanamke wa kumi na saba katika historia ya Tuzo ya Nobel ya Fasihi na anamrithi mwandishi wa riwaya wa Tanzania Abdulrazak Gurnah ambaye mwaka 2021 alikuwa Mwafrika wa tano kutunukiwa tuzo hiyo.

Katika enzi ya mitandao ya kijamii na shinikizo la upesi kwenye maisha yetu, ishara kubwa ya kwanza ya mshindi haikuweza kufikiwa. Kamati ya Tuzo ya Nobel imetangaza jina la Annie Ernaux, lakini wakati huo huo, ilibidi ikiri kwamba haikuweza kumpata mshindi huyo kwa njia ya simu.

"Nguvu ya ukombozi ya uandishi"

Hatimaye, televisheni ya Sweden SVT ndiyo ambayo iliweza kuwasiliana na mshindi. Kwa hivyo, Annie Ernaux alizungumza juu ya "heshima kubwa sana" na "wajibu". "Akimaanisha kushuhudia [...] kwa aina ya haki, ujasiri, ikilinganishwa na juinsi ilivyo dunia".

Annie Ernaux, ambaye anapelekea kwa sasa Ufaransa kuwa na idadi ya washindi kumi na sita, alizaliwa mwaka wa 1940 huko Lillebonne na alikulia kwenye umbali wa kilomita kahaa, huko Yvetot, katika mazingira ya kawaida ambayo anashuhudia katika kitabu chake cha kwanza, Les armoires vides, uchunguzi kuhusiana na chimbuko lake (kutoka Normandy), kilichochapishwa mwaka wa 1974. Kwa muda mrefu alikuwa na aibu kwa wazazi wake ambao walikuwa na duka la mboga na kuuza kahawa katika mji huu mdogo karibu na pwani ya Normandy. Ili kuwa mwandishi, Ernaux alilazimika kusafiri njia ndefu na ngumu. Katika riwaya zake, mwandishi mara kwa mara anaibua maisha haya katika mazingira ya mashambani yaliyo na alama za jinsia, lugha na tabaka la kijamii. Kwake, uandishi wake, uliojaliwa mtindo ambao ni wa kawaida na wa angavu, mgumu na wa uwazi, unalenga kupanua mipaka ya fasihi zaidi ya hadithi za uwongo na masimulizi ya kimapenzi. Yeye mwenyewe alijieleza kama "mtaalamu wa ethnolojia" akidokeza kimakusudi kazi muhimu sana za mwanasosholojia Pierre Bourdieu, lakini pia kazi bora ya Marcel Proust, In Search of Lost Time.

Mwandishi wa "Tukio" na "Miaka"

Miongoni mwa kazi bora za Annie Ernaux ni "L’événement (2000)", iliyorushwa hewani hivi majuzi kwenye televisheni na mtayarishaji wa makala, ambaye ni raia wa Ufaransa mwenye asili ya Lebanon, Audrey Diwan, na kutunukiwa tuzo ya Simba ya Dhahabu kwenye Tamasha la Filamu la Venice mnamo 2021. Katika simulizi hii iliyosafishwa ya mtu wa kwanza, Ernaux anatumia fasihi kama silaha kali ya kupotosha ukweli. Anatuongelea historia yake ya kutoa mimba kwa siri, akiwa na umri wa miaka 23, katika Ufaransa ya kitamaduni na kandamizi ya miaka ya 1960.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.