Pata taarifa kuu
VATICAN-KANISA-KASHFA YA NGONO

Kardinali George Pell akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto

Mahakama ya Australia imemkuta na hatia ya unyanyasaji wa kijinsi dhidi ya watoto kiongozi wa hadhi ya juu wa Kanisa Katoliki, Kardinali kutoka Australia George Pell.

Kardinali George Pell katika mahakama ya Melbourne, Februari 26, 2019.
Kardinali George Pell katika mahakama ya Melbourne, Februari 26, 2019. AAP Image/David Crosling/via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mashitaka yalifunguliwa tangu Desemba 11 mwaka jana, lakini vyombo vya habari vilikuwa vimepigwa marufuku kutoa taarifa hiyo baada ya kutahadharishwa kufunguliwa mashitaka. Lakini pamoja na kuondolewa kwa marufuku hiyo, Jumanne wiki hii, taarifa hiyo imetangazwa kwenye vyombo vya habari.

Kardinali George Pel amekutwa na hatia, ikiwemo ya kumuingilia mtoto wa umri ulio chini ya miaka 16, na hatia zingine nne za kuwafanyia vitendo visivyo vya kawaida watoto wa chini ya miaka 16.

Hata hivyo Kardina Pell amekanusha tuhuma hizo dhidi yake .

Pell mwenye umri wa miaka 77 anatarijiwa kuhukumiwa siku ya Jumatano, lakini mawakili wake wanasema kua watakata rufaa hatia hiyo.

Kardinal George Pell ambaye ni kiongozi wa kanisa aliyekuwa anashikilia nafasi ya Muweka hazina, ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu zaidi kanisani.

Kanisa Katoliki duniani kote kwa miaka ya hivi karibuni, limeendelea kukumbwa na kashfa ya unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto, na kudaiwa kuwa wamekua wakificha masuala hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.