Pata taarifa kuu
DRC-PAPA WEMBA

Côte d'Ivoire yajiandaa kuusafirisha mwili wa Papa Wemba

Mji mkuu wa Cote d'Ivoire unajiandaa kusafirisha mwili wa Papa Wemba. Mfalme wa Rumba ya Congo alifariki usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili. Alikuwa na umri wa miaka 66.

Papa Wemba kwenye tovuti ya FEMUA, tamasha la muziki unaochezwa katika miji ya Anoumabo.
Papa Wemba kwenye tovuti ya FEMUA, tamasha la muziki unaochezwa katika miji ya Anoumabo. © DR
Matangazo ya kibiashara

Papa Wemba, mzaliwa wa Matonge (moja ya kata maarufu mjini Kinshasa) alianguka na kupoteza fahamu wakati wa tamasha la Jumamosi usiku. Ilikuwa katika mji mkuu Abidjan, nchini Cote d'Ivoire, wakati wa Sherehe ya muziki unaochezwa katika miji ya Anoumabo. Leo huzuni na hisia vimetawala ulimwengu wa muziki na bara nzima la Afrika.

Tarehe sahihi ya kusafirishwa mwili wa Papa Wemba itafahamika leo mchana. waandaaji wa sherehe hiyo FEMUA, tamasha la muziki unaochezwa katika miji ya Anoumabo na mamlaka ya Cote d'Ivoire wanaendelea kushughulikia suala hili.

Jumapili usiku, wanamuziki 22 na waimbaji wa Papa Wemba wamekua wakiomba kurudi haraka iwezekanavyo mjini Kinshasa. Lakini waandaaji wa tamasha hilo walikua bado na tatizo la kupata nafasi katika ndege.

Salif Traoré, Kamishna wa FEMUA, pia anataka kuandaa mjini Anoumabo kwenye jukwaa la tamasha, mkesha mkubwa ambapo wasanii wa Cote d'Ivoire watakuja kutoa heshima zao za mwisho kwa mfalme wa Rumba aliefariki Jumapili asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.