Pata taarifa kuu
UE-UGAIDI-USALAMA

EU: utaratibu mpya dhidi ya ugaidi wapitishwa

Muswada wa maelekezo kuhusu daftari la Ulaya la data za abiria wanaosafiri kwa ndege, ujulikanao kama Passenger Name Record au « PNR », umepitishwa Alhamisi hii Aprili 14 na bunge la Ulaya mjini Strasbourg.

Bunge la Ulaya mjini Strasbourg.
Bunge la Ulaya mjini Strasbourg. REUTERS/Jean-Marc Loos
Matangazo ya kibiashara

PNR ni chombo kipya kitakachotumiwa kwa kupambana dhidi ya ugaidi. Chombo hiki kilichoombwa na baadhi ya nchi za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa.

Moja ya mambo muhimu ya ajenda ya kikao cha mjadala kwenye Bunge la Ulaya mjini Strasbourg ilikuwa, Jumatano hii mchana, mjadala juu ya maelekezo kuhusu "matumizi ya data za faili za abiria", yanayojulikana zaidi kwa ufupi kwa lugha ya Kingereza kama "PNR" (Passenger Name Record). Kazi kuhusu "maelekezo ya PNR" ilichelewa kwa miaka kadhaa. Mchakato ulianzishwa ghafla wakati wa kikao maalum cha Bunge la Ulaya.

Jumatatu wakati kikao hiki kilianza, kura kuhusu maelekezo bado imepangwa katika kikao kijacho cha Bunge mwezi Mei. Lakini shinikizo la matukio, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya hivi karibuni mjini Paris na Brussels, lilikua kubwa mno. Makundi makuu ya Wabunge yalikubaliana juu ya utaratibu wa kasi na kuamua kuingiza upigaji kura kuhusu maelekezo ya PNR katika ajenda ya kikao cha Alhamisi wiki hii.

Kabla ya mfululizo wa hivi karibuni wa mashambulizi, mjadala ulikua kwa sehemu kubwa umezorota kwa hofu ya kutishia uhuru wa msingi kwa kufichua data binafsi za abiria wanaosafiri kwa ndege, ikimaanisha, mamilioni ya wananchi wa Ulaya - kwa huduma za usalama barani Ulaya, laikini pia kwingineko, ikiwa ni pamoja na Marekani. Tangu mashambulizi mabaya yaliosababisha vifo vingi barani Ulaya, haja ya kubadilishana taarifa inaonekana si tu kueleweka vema, lakini inachukuliwa kama ya haraka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.