Pata taarifa kuu

Tuzo ya Marc-Vivien Foé mwaka wa 2024

Tuzo ya RFI-FRANCE 24 kumuenzi aliyekuwa mchezaji wa Marc-Vivien Foé, aliyewahi kuichezea klabu ya Lyon, raia wa Cameroon kabla ya kifo chake uwanjani mwaka 2003.

Wachezaji wanaowania Tuzo ya Marc-Vivien Foé mwaka wa 2024
Wachezaji wanaowania Tuzo ya Marc-Vivien Foé mwaka wa 2024 © Studio graphique FMM
Matangazo ya kibiashara

Tuzo hii imekuwa ikitolewa kila mwaka tangu mwaka 2009, kwa mchezaji kutoka barani Afrika, aliyefanya vizuri kwenye ligi ya soka nchini Ufaransa.

Mshindi wa msimu wa mwaka 2023/24 atafahamika tarehe 13 mwezi huu.

Wachezaji watatu wanaowania tuzo hiyo ni pamoja :

Pierre-Emerick Aubameyang, Mshambuliaji (Gabon/Marseille) 

Aliwahi kushinda tuzo hili mwaka wa 2013 wakati akiichezea klabu ya AS Saint-Étienne na amekuwa na msimu bora tangu kujiunga na Marseille kama mchezaji huru.

Kwa sasa ana magoli 22 katika mashindano yote.

Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon.
Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon. AFP - CLEMENT MAHOUDEAU

Nabil Bentaleb - LOSC Lille/Algeria

Licha ya timu yake ya taifa kuondolewa mapema katika mashindano ya AFCON mwaka huu, ameonyesha mchezo bora na klabu yake licha ya kukabiliwa na jeraha, mchezo wake umeonekana kumvutia kocha wake Paulo Fonseca.

Nabil Bentaleb
Nabil Bentaleb Wolfgang Rattay/Reuters

Achraf Hakimi - Paris Saint-Germain/Morocco

Achraf Hakimi - Paris Saint-Germain/Morocco
Achraf Hakimi - Paris Saint-Germain/Morocco PSG via Getty Images - Aurelien Meunier - PSG

Hakimi licha ya kuonyesha mchezo bora na timu yake ya taifa katika mechi za Afcon, amekuwa nguzo muhimu kwa kikosi cha kocha Luis Enrique.

Soma piaDRC: Chancel Mbemba ndiye mshindi wa tuzo za Marc-Vivien Foé 2023

Tuzo ya msimu uliopita, ilimwendea Chancel Mbemba, kutoka klabu ya Marseille, raia wa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.