Pata taarifa kuu

Kylian Mbappe athibitisha kuondoka PSG mwishoni mwa msimu huu

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Kylian Mbappe, Ijumaa ya wiki hii amethibitihsa kuwa ataondoka katika klabu ya Paris St-Germain mwishoni mwa msimu.

Mkataba wake na klabu ya PSG unatarajiwa kukamilika mwezi Juni ambapo amekuwa akihusishwa na kuhamia katika klabu ya Real Madrid.
Mkataba wake na klabu ya PSG unatarajiwa kukamilika mwezi Juni ambapo amekuwa akihusishwa na kuhamia katika klabu ya Real Madrid. © AFP - FRANCK FIFE
Matangazo ya kibiashara

Mbappe, mwenye umri wa miaka 25, alithibitisha kuondoka kwake PSG kupitia video alizochapisha kwenye mitandao yake ya kijami.

"Nimekuwa niwaeleza kwamba ntazungumza nanyi muda utakapofika’’ alisema Mbappe.

"Ni mwaka wangu wa mwisho katika klabu ya Paris St-Germain. Sitaongeza mkataba wangu na muda wangu hapa utafikia kikomo katika kipindi cha wiki chache zijazo.”

Mkataba wake na klabu ya PSG unatarajiwa kukamilika mwezi Juni ambapo amekuwa akihusishwa na kuhamia katika klabu ya Real Madrid ya nchini Uhispania.

Mbappe, mshindi wa kombe la dunia akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa, amefanikiwa kuifungia PSG mabao 255 na anatarajiwa kucheza mechi yake ya mwisho akiwa na PSG siku ya Jumapili dhidi ya Toulouse katika Ligue 1.

Aidha ameeleza kuwa klabu ya PSG imemsaidia pakubwa katika taaluma yake ya soka baada ya kujiunga nayo kwa kima cha Euro Milioni 165.7 akitoa katika klabu ya Monaco ya nchini Ufaransa mwezi Agosti mwaka wa 2017.

Nyota huyo wa Ufaransa ameisadia pakubwa timu yake ya taifa katika kombe la dunia.
Nyota huyo wa Ufaransa ameisadia pakubwa timu yake ya taifa katika kombe la dunia. REUTERS - BERNADETT SZABO

Mbappe alitarajiwa kuondoka PSG kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu wa mwaka wa 2021-22 lakini akaongeza mkataba wa miaka miwili, akipewa nafasi ya kuongeza mkataba mwengine wa mwaka mmoja mwaka huu.

Mbappe alikutana na rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi mnamo Februari 13 na kumwambia kuwa anaondoka akiwa na lengo la na kujiunga na Real.

Kylian Mbappé amefanikiwa kuifungia PSG mabao 255.
Kylian Mbappé amefanikiwa kuifungia PSG mabao 255. AFP - FRANCK FIFE

PSG ilipokea kichapo cha jumla cha mabao 2-0 kutoka kwa Borussia Dortmund katika nusu fainali mapema wiki hii ya kuwania klabu bingwa barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.