Pata taarifa kuu

Brazil kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la wanawake la mwaka 2027

Brazil itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la kwanza la wanawake litaloandaliwa Amerika Kusini mnamo 2027, Shirikishola Soka Suniani, FIFA limetangaza leo Ijumaa, katika kikao chake huko Bangkok. Faili ya Brazil ilishinda ugombea wa pamoja wa Ujerumani, Ubelgiji na Uholanzi, kwa kura 119 dhidi ya 78 za mashirikisho wanachama.

Mechi ya ufunguzi na fainali zitapigwa katika uwanja wa Maracana mjini Rio.
Mechi ya ufunguzi na fainali zitapigwa katika uwanja wa Maracana mjini Rio. AP - Felipe Dana
Matangazo ya kibiashara

"Ninahisi kuguswa sana, tunajua itakuwa vigumu sana. Ni ushindi kwa soka ya Amerika Kusini, na kwa soka ya wanawake katika Amerika Kusini," amesema Mkuu wa Shirikisho la Soka la Brazil, Ednaldo Rodrigues. Kwa toleo lake la kumi, shindano hilo linajiandaa kuchunguza bara jipya, baada ya mafanikio mnamo mwaka 2023, huko Australia na New Zealand, ambayo yalivunja rekodi za kibiashara na watazamaji, katika muundo na timu 32 zilizotumiwa kwa mara ya kwanza.

Mashindano ya kuandaa mashindano makubwa ya soka yamekuwa nadra. Matoleo ya 2028 na 2032 ya Euro ya wanaume yaliwekwa mwaka jana kwa faili moja, ikisubiri Kombe la Dunia la mwaka 2030 na 2034 ambapo mshindani mmoja tu anaonekana kila wakati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.