Pata taarifa kuu

Timu za Kenya za Talanta Hela U19 zafanya vizuri nchini Uhispania

Nairobi – Timu za Talanta Hela U19 za Kenya zimefanya vizuri katika ufunguzi wa Costa Daurada Cup huko Tarragona, Hispania. Vijana hawa wameonyesha ustadi na azma , wakiwashinda wapinzani wao kwa ushindi wa kuvutia. Mashabiki wanangoja kwa hamu mechi zijazo, huku timu za Kenya zikilenga kuendeleza rekodi yao nzuri na kuhamasisha vizazi vijavyo vya nyota za soka.

Timu ya vijana wa kiume ya kenya mazoezini kabla ya mechi.
Timu ya vijana wa kiume ya kenya mazoezini kabla ya mechi. © Tabitha Nashipae - Ministry of sports Kenya.
Matangazo ya kibiashara

Timu za soka za vijana chini ya umri wa miaka 19 za Talanta Hela kutoka Kenya zimeonyesha uwezo mkubwa katika siku ya kwanza ya mashindano ya Costa Daurada huko Tarragona, Hispania.

 

Wizara ya Michezo nchini Kenya yasherehekea kufanya vizuri kwa timu za vijana

Timu za Kenya zaanza mashindano kwa ushindi

Vijana hawa kutoka Kenya wameonyesha ustadi wao kwa kuwashinda wapinzani wao kwa ushindi wa kuvutia.

Timu ya wavulana ilianza vizuri kampeni yao kwa kushinda mchezo wao wa kwanza kwa mabao 3-0 dhidi ya CF Constantine kwenye Uwanja wa CD Riudoms. Mabao kutoka kwa Alex Kipruto, Elisha Nalianya, na Derrick Oketch yaliisaidia timu kushinda kwa kujiamini.

Timu ya vijana wa kiume ya Kenya kabla ya kuanza kwa mechi baina yao na CF Constantine.
Timu ya vijana wa kiume ya Kenya kabla ya kuanza kwa mechi baina yao na CF Constantine. © Tabitha Nashipae - Ministry of sports Kenya.

Bila kuvunjika moyo na changamoto za kuzoea mazingira na hali ya hewa isiyozoeleka, wavulana waliongeza rekodi yao ya ushindi kwa kuwashinda

Kocha wa timu, Stanley Okumbi, aliwapongeza wachezaji kwa utendaji wao wa kipekee na akasisitiza umuhimu wa mashindano kama haya katika kutoa fursa na uzoefu muhimu kwa vijana.

Wakati huo huo, timu ya wasichana ya Talanta Hela U19 iliendeleza utawala wao uwanjani kwa kuwashinda CE Jupiter kwa ushindi wa kuvutia wa mabao 4-0 katika mchezo wao wa kwanza.

 

Timu ya vijana wa kike ya kenya nchini Uhispania kabla ya mechi dhidi ya CE Jupiter.
Timu ya vijana wa kike ya kenya nchini Uhispania kabla ya mechi dhidi ya CE Jupiter. © @Ministry of sports, Kenya

Mabao kutoka kwa Elizabeth Mideva, Marion Musanga, na Hilda Natecho yalionyesha vipaji na ujuzi wa wasichana wa Kenya na hii ilipata pongezi kutoka kwa kocha wao, Jackline Juma.

Ushindi katika siku ya kwanza ya Costa Daurada Cup unathibitisha juhudi na kujitolea kwa vijana hawa wa soka kutoka Kenya.

Mafanikio ya miradi kama vile mashindano ya Talanta Hela U19 yanasisitiza dhamira ya nchi katika kukuza na kuendeleza vipaji vya michezo.

Mashindano yakiendelea, timu za wavulana na wasichana zinatarajiwa kuendeleza utendaji wao wa kuvutia, na mechi za kusisimua dhidi ya wapinzani wenye nguvu zinazofuata.

Costa Daurada Cup hutoa jukwaa kwa wachezaji vijana kutangaza vipaji vyao na pia kuchochea ushirikiano na ushindani kimataifa miongoni mwa vijana zaidi kutoka kote duniani.

Wapenzi wa soka wanatazamia kwa hamu mechi zijazo, huku timu za Kenya zikilenga kuiweka nchi yao kwenye ramani ya kimataifa na kuhamasisha vizazi vijavyo vya nyota za soka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.