Pata taarifa kuu

Mvutano kati ya Rwanda na Burundi waivaa BAL

Timu ya Burundi ya Mpira wa Kikapu ya Dynamo Club imeondolewa kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu barani Afrika kwa kukataa nembo ya "Visit Rwanda" mdhamini wa mashindano hayo kuonekana kwenye jezi yake.

Mechi ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basket Africa League) mjini Kigali, Rwanda, Mei 27, 2021.
Mechi ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basket Africa League) mjini Kigali, Rwanda, Mei 27, 2021. © LUDOVIC MARIN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwisho wa matukio kwa Klabu ya Mpira wa Kikapu ya Dynamo Club katika Ligi ya Mpira wa Kikapu barani Afrika (BAL). Licha ya ushindi wa kwanza siku ya Jumamosi Machi 9, 2024 dhidi ya Cape Town Tigers ya Afrika Kusini (86 hadi 73) huko Pretoria kama sehemu ya Mkutano wa Kalahari, timu ya Burundi haitacheza michuano mingine.

Siku ya Jumanne Machi 12 klabu ya Mpira wa Kikapu ya Dynamo Club ilitengwa na waandaaji kwa kukiuka kanuni zinazohusu jezi na sare za michuano hiyo. Sababu, Ni kwa mara ya tatu kwa klabu ya Mpira wa Kikapu ya Burundi Dynamo Club kukataa kuvaa jezi zenye nembo ya "Visit Rwanda", mdhamini wa michuano hii.

"Klabu ya Mpira wa Kikapu ya Dynamo Club ilikataa kufuata sheria na matakwa ya jezi na sare za Ligi ya Mpira wa Kikapu barani Afrika, na kusababisha kufungiwa mechi yake ya leo dhidi ya Petro de Luanda (Angola) na kupoteza ushiriki wake katika msimu wa 2024 BAL", Tume inayoaandaa michuano hiyo, kupitia mwenyekiti wake Amadou Gallo Fall, imetangaza.

Uamuzi huu unakuja baada ya klabu hiyo tayari kukataa kucheza mechi yake ya awali, siku mbili mapema kwa sababu hiyo hiyo. "Serikali ilimwambia kiongozi wetu kwamba hatungeweza kucheza. Waliiambia BAL kwamba tunapaswa kupoteza kwa sababu hatuwezi kuvaa jezi zenye nembo iliyoandikwa 'Visit Rwanda," amesema Bryton Hobbs, mmarekani, mmoja wa wachezaji wa Dynamo Club alieleza wakati huo moja kwa moja kwenye Instagram.

"Chini ya sheria za FIBA, kupoteza mara mbili katika mashindano hayo husababisha kufungiwa michezo moja kwa moja kwa kilabu," amesema mkuu wa BAL, akitaja "hali ya kusikitisha sana kwa mashabiki na wachezaji".

Mshirika wa kihistoria wa BAL tangu kuanza kwake mwaka 2021 na shirika la ndege la kitaifa la RwandAir, Visit Rwanda ni tawi la utalii la Bodi ya Maendeleo ya Rwanda, chombo cha serikali ya Rwanda kinachohusika na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi ya nchi hii ya Maziwa Makuu.

Mvutano wa mara kwa mara

Pia itaandaa awamu za mwisho za shindano hilo kuanzia Mei 24 hadi Juni 1 katika mji mkuu, Kigali. Ukweli unabaki kuwa nchi hiyo na jirani yake Burundi zinakabiliwa na uhusiano wa wasiwasi, unaoonyeshwa haswa na shutuma za pande zote za kuvuruga utulivu na kufungwa mwanzoni mwa mwezi wa Januari 2024 kwa mipaka yote upande wa Burundi.

Visit Rwanda imeanzisha ushirikiano katika soka la Afrika na Ulaya, zikiwemo Arsenal, Paris Saint-Germain na Bayern Munich. Hii si mara ya kwanza kwa taasisi hii kukumbwa na msuguano kati ya taifa la Rwanda na majirani zake. Klabu ya TP Mazembe kutoka DRC pia ilikataa mnamo Oktoba 2023 kuwezesha nembo hii ionekane kwenye jezi yake kama sehemu ya Ligi ya Soka ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.