Pata taarifa kuu

Aliou Cissé aongezwa muda kuinoa timu ya taifa ya senegal hadi mwaka 2026

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Senegal, Aliou Cissé, ameteuliwa tena kuendelea kuinoa timu hiyo hadi Kombe la Dunia la 2026, Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) lilitangaza kwenye video iliyorushwa hewani siku ya Ijumaa.

Kocha wa Senegal Aliou Cissé katika mkutano na waandishi wa habari katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Qatar (QNCC) huko Doha mnamo Novemba 24, 2022, mkesha wa mechi ya soka ya Kombe la Dunia la Qatar 2022 kati ya Qatar na Senegal.
Kocha wa Senegal Aliou Cissé katika mkutano na waandishi wa habari katika Kituo cha Mikutano cha Kitaifa cha Qatar (QNCC) huko Doha mnamo Novemba 24, 2022, mkesha wa mechi ya soka ya Kombe la Dunia la Qatar 2022 kati ya Qatar na Senegal. © OZAN KOSE / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Kamati ya utendaji (ya shirikisho) inaongeza imani yake kwa kocha Aliou Cissé na inamtaka aendelee na misheni yake kwa nia ya kufikia malengo ya siku zijawaka 2026", alitangaza makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Senegal, Seydou Sane.

Timu ya Simba ya Teranga inatoka katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kubandulia katika hatua ya 16 bora na mwenyeji na mshindi wa michuano hiyo, Côte d'Ivoire.

Chini ya maagizo ya Aliou Cissé, 47, kocha wa Simba wa Teranga tangu mwaka 2015, Senegal ilishinda AFCON kwa mara ya kwanza katika historia yake wakati wa toleo lililoshindaniwa mnamo 2022, baada ya kufika fainali ya shindano la bara hilo mnamo mwaka 2019.

Kwa sasa Senegal iko katika nafasi ya 17 katika viwango vya FIFA, ikiwa nafasi ya pili kwa ubora kwa timu za Afrika baada ya Morocco (ya 12).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.