Pata taarifa kuu

Wanariadha wa kenya kumuenzi Kiptum katika mbio za Olimpiki jijini Paris

Nairobi – Rais wa Kenya William Ruto, aliyeongoza maelfu ya waombolezaji katika uwanja wa maonyesho wa Chepkorio eneo bunge la Keiyo Kusini, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, amewataka wanariadha wa Kenya watakaoshiriki katika Michezo ya olimpiki Paris kushinda medali kwa wingi kama ishara ya heshima kwa mwanariadha wa mbio za marathon mwendazake Kelvin Kiptum.

Kelvin Kiptum amezikwa nyumbani kwake katika kaunti ya Uasin Gishu
Kelvin Kiptum amezikwa nyumbani kwake katika kaunti ya Uasin Gishu REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Kenya William Ruto, amewataka wanariadha wa Kenya watakaoshiriki katika Michezo ya olimpiki Paris kushinda medali kwa wingi kama ishara ya heshima kwa mwanariadha wa mbio za marathon mwendazake Kelvin Kiptum.

Mazishi ya mwanariadha huyo yalihudhuriwa na idadi kubwa ya wakenya
Mazishi ya mwanariadha huyo yalihudhuriwa na idadi kubwa ya wakenya REUTERS - STRINGER

Rais Ruto ambaye aliongoza maelfu ya waombolezaji katika uwanja wa maonyesho wa Chepkorio eneo bunge la Keiyo Kusini, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, aliongeza kuwa matarajio ya Kiptum kutawala mbio za marathon kwa miaka mingi ijayo yalikuwa wazi.

"Ninajua kuwa sote tulikuwa na matumaini kwamba Kiptum angeiweka Kenya katika ramani ya kimataifa hata katika Olimpiki zijazo huko Paris, lakini kwa kuwa tuna nyinyi wanariadha wetu na mmesikia kutoka kwetu sote, Paris itakuwa Olimpiki ya kumuenzi huyu Kelvin. Tunataka muifanye Paris kuwa Olimpiki ya Kelvin Kiptum.”

Wito wa Ruto pia ulisisisitizwa na rais wa shirikisho la Riadha nchini Kenya Jackson Tuwei na rais wa Kamati ya Kitaifa ya Olimpiki ya Kenya (NOC-K) Paul Tergat, wakisema kwamba jamii ya wanariadha imepoteza bingwa wa dunia katika umri wa miaka 24.

Tuwei alisema maendeleo ya Kiptum katika mbio za marathon yalikuwa ya kushangaza.

 

"Tulipochanganua maendeleo katika mbio za nusu marathon na mbio zote mbili alizokimbia, dalili zote zilionyesha kwamba bila shaka angetimiza ndoto yake ya kukimbia mbio hizo chini ya saa mbili."

“Tulikuwa tumechagua timu ya wanariadha wa kiume na wa kike wa marathon kuwakilisha Kenya na jina lake lilikuwa juu ya orodha hiyo. Tutamkosa huko Paris,’’ akaongeza Tuwei.

 

Itakumbukwa kuwa Kiptum alifariki katika ajali ya barabarani pamoja na kocha wake raia wa Rwanda Gervais Hakizimana.

Gari alilokuwa akisafiria Kiptum
Gari alilokuwa akisafiria Kiptum REUTERS - STRINGER

Waziri wa michezo nchini Kenya Ababu Namwamba alizuru Rwanda kwa ziara ya siku mbili na kudhibitisha kua serikali ya kenya imetoa msaada kwa familia ya Mwenda zake Hakizimana.

00:33

Ababu Namwamba- Waziri wa Michezo, Kenya

Kiptum alizikwa Ijumaa kwake nyumbani katika kijiji cha Naiberi katika Kaunti ya Uasin Gishu baada ya hafla ya mazishi kufanywa katika uwanja wa Chepkorio kaunti ya Elgeiyo Marakwet.

Mwanariadha huyo alikua baba wa watoto wawili na mme wa mke mmoja mjane Asenath Rotich Kiptum.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.