Pata taarifa kuu

Ujerumani: Toni Kroos atangaza kurejea kwenye timu yake ya taifa

Mshindi wa Kombe la Dunia la 2014 akiwa na Mannschaft, kiungo wa kati wa Real Madrid Toni Kroos ametangaza kurejea kwenye timu yake siku ya Alhamisi, wiki chache kabla ya kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya, Euro-2024.

Toni Kroos akikimbia wakati wa mechi ya UEFA EURO 2020 kati ya Uingereza na Ujerumani, London, Juni 29, 2021.
Toni Kroos akikimbia wakati wa mechi ya UEFA EURO 2020 kati ya Uingereza na Ujerumani, London, Juni 29, 2021. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

"Vipi vijana, ili kuwaeleza haraka, nitaichezea tena timu ya taifa ya Ujerumani kuanzia mwezi Machi. Kwa nini? Kwa sababu kocha ameniomba, na kwa sababu niko tayari", ameandika kwenye Instagram mchezaji huyo, ambaye ana kufikia sasa amevichezea vilabu 106na alitangaza kumaliza kazi yake ya kimataifa mnamo mwaka 2021.

"Nina uhakika tunaweza kufanya vyema zaidi tukiwa na timu hii kwenye michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya kuliko watu wengi wanavyofikiria leo," ameongeza.

Mnamo mwezi wa Desemba, kocha wa Ujerumani Julian Nagelsmann aliibua uwezekano wa kumrejesha kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34, ili kuleta uzoefu kwenye timu hii ya taifa ya Ujerumani ambayo iko katika hali mbaya baada ya kumalizika kazi yake kimataifa katika kikosi hake kilichotawazwa mabingwa wa dunia mwaka wa 2014.

Ujerumani litamenyana na Ufaransa na Uholanzi katika mechi ya kirafiki mwezi wa Machi wiki ijayo, kabla ya Euro "yake" nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.