Pata taarifa kuu

Ivory Coast ndio mabingwa wa Afcon 2023

Nairobi – Goli la mshambuliaji wa klabu ya Borrusia Dortmund ya nchini Ujerumani, Sebastien Haller, hapo jana lilitosha na kusaidia timu yake ya taifa ya Ivory Coast, kushinda taji la michuano ya kombe la mataifa ya Afrika dhidi ya Nigeria, katika mchezo wa fainali uliochezwa Abdijan.

Ivory Coast waliishinda Nigeria 2-1
Ivory Coast waliishinda Nigeria 2-1 PIERRE RENE-WORMS/FMM
Matangazo ya kibiashara

Ni ushindi ambao uliwafanya mashabiki wa Ivory Coast kushangilia kama watu wenye wazimu, ikiwa ni taji lake la tatu baada ya kufanya hivyo mwaka 1992 na 2015.

Nigeria ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kutwaa taji hilo, ndio iliyotangulia kupata goli, na ikaonekana ni kana kwamba inaweza kuwa marudio ya ushindi iliyoupata dhidi ya wenyeji hao katika hatua ya makundi.

Hata hivyo, furaha ya Super eagles ilizimwa na Frank Kessie aliyeisawazishia timu yake, kabla ya dakika ya 81, Sebastien Haller kutumia vema pasi aliyopewa na Simon Adingra, kukamilisha ndoto ya timu hiyo.

Ivory Coast imekuwa timu ya kwanza kushinda taji hilo katika ardhi ya nyumbani, tangu Misri ilipofanya hivyo mwaka 2006 ilipokuwa mwenyeji wa michuano hiyo, ambapo iliifunga Ivory Coast kwa njia ya penalti na wakati huo nahodha wake akiwa Didier Drogba.

Idadi kubwa ya mashabiki wa Ivory Coast walijitokeza kuishabikia timu yao
Idadi kubwa ya mashabiki wa Ivory Coast walijitokeza kuishabikia timu yao PIERRE RENE-WORMS/FMM

Hata hivyo haikuwa michuano mizuri kwa mshambuliaji kinara wa Nigeria, Victor Osimhne, ambaye amefunga goli 1 pekee katika mechi 7 alizocheza.

Michuano hii imetamatika huku ikiwa imeweka historia kwa kushuhudia timu zenye uzoefu kama Cameroon, Misri na Morocco zikiaga mashindano hayo katika hatua ya makundi.

Nigeria ilimaliza ya pili ikifuatiwa na DRC
Nigeria ilimaliza ya pili ikifuatiwa na DRC PIERRE RENE-WORMS/FMM

Kwa ukanda wa Afrika Mashariki, wakazi wengi wanajivunia kiwango cha DRC licha ya kushindwa katika hatua ya nusu fainali na ile ya mshindi watatu, huku kwa wawakilishi wengine wa ukanda huo, timu ya taifa ya Tanzania, watakuwa na lakujifunza baada ya kuaga katika hatua ya makundi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.