Pata taarifa kuu

AFCON: Kocha wa Côte d'Ivoire ataka "kombe kubaki nyumbani"

Kocha wa Côte d'Ivoire, Emerse Faé, ambaye alichukua wadhifa huo katikati mwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, anataka "kombe hili kubaki nyumbani", amesemasiku ya  Jumamosi usiku wa kuamkia siku ya mechi ya fainali nyumbani dhidi ya Nigeria.

Kocha wa Côte d'Ivoire Emerse Fae katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jumba la utamaduni mjini Abidjan..
Kocha wa Côte d'Ivoire Emerse Fae katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Jumba la utamaduni mjini Abidjan.. © Pierre René-Worms/RFI
Matangazo ya kibiashara

 

"Kesho (Jumapili saa tatu usiku katika mjini Abidjan), tutakuwa na dakika 90 kabla ya kuongeza nyota wa tatu kwenye jezi ya chungwa ya Côte d'Ivoire" baada ya kutawazwa kwa mwaka wa 1992 na 2015, amebainisha katika mkutano na waandishi wa habari.

"Ikiwa uko katika fainali, ni kwa sababu unastahili," amesema Faé wakati wa kukabiliana na hatua ya mwisho ya safari ambayo wakati mwingine imekuwa muujiza. Emerse Faé alichukua nafasi ya Mfaransa Jean-Louis Gasset ambaye alikuwa akiinoa timu hii ya Côte d'Ivoire baada ya hatua ya makundi.

"Tembo" walikuwa wamemaliza duru hii ya kwanza kwa kichapo kikali cha mabao 4-0 dhidi ya Equatorial Guinea, na, ya tatu katika kundi lao, ilinyakua tikiti ya mwisho ya hatua ya 16 bora. "Tumetoka mbali," alithibitisha mshambuliaji Sébastien Haller. "Kila mtu alipitia nyakati ngumu sana baada ya kushindwa dhidi ya Equatorial Guinea."

“Tulibahatika kupata la pili (bahati), ni juu yetu kutoa upeo na zaidi ya yote tusiwe na majuto, hilo ndilo lililosaidia kulibana kundi hili, tukijua kwamba tumepita karibu ndoto mbaya. Kisichokuua kinakufanya uwe na nguvu zaidi", alimalizia mshambuliaji huyo.

Kwa upande wake, kocha wa Nigeria, Mreno José Peseiro, amerudia mara kadhaa kuwa anataka "kushinda AFCON hii". "Ni vizuri sana kufika hapa, lakini kuna mechi moja iliyosalia, na hiyo ndiyo muhimu zaidi," alisema tena Jumamosi. Inayoitwa mnamo mwaka wa 1980, 1994 na 2013, timu yake Super Eagles watawania nyota ya nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.