Pata taarifa kuu
SYRIA-MAPIGANO

Zaidi ya watu 300 wameuawa katika mapigano Damascus

Mapigano makali kwa siku ishirini kati ya makundi hasimu ya wapiganaji wa Kiislamu kwa kudhibiti ngome ya waasi karibu na mji wa Damascus yamewaua zaidi ya watu 300, shirika lisilo la kiserikali limearifu Jumapili hii.

Mapigano makali kati ya waasi na serikali yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Douma, karibu na mkoa wa Damascus, Februari 27, 2016.
Mapigano makali kati ya waasi na serikali yamesababisha uharibifu mkubwa katika eneo la Douma, karibu na mkoa wa Damascus, Februari 27, 2016. REUTERS/Bassam Khabieh
Matangazo ya kibiashara

Mapigano katika eneo la Ghouta mashariki, mashariki mwa mji mkuu wa Syria, kati ya kundi la Jaich al-Islam, upande mmoja, kundi linalotii nadharia ya Kisalafi linaloungwa mkono na Saudi Arabia na ambalo lilishiriki katika mazungumzo ya amani mjini Geneva, na upande mwengine, muungano kati ya kundi la Faylaq al-Rahman, kundi jingine la wapiganaji wa Kiislamu na kundi la al-Nosra Front lenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda nchini Syria.

"Wapiganaji zaidi ya 300 kwa pande zote mbili, na raia zaidi ya kumi wameuawa katika mapigano ya kudhibiti eneo la Ghouta tangu Aprili 28," Rami Abdel Rahman, mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu nchini Syria (OSDH) ameliambia shirika la habari la AFP.

Vijiji kadhaa katika eneo la Ghouta, ngome muhimu ya waasi katika jimbo la Damascus, vinashikiliwa na majeshi ya Bashar al-Assad.

Mkataba wa usitishwaji wa mapigano kati ya serikali na waasi ulioafikiwa nchini Syria tangu mwishoni mwa mwezi Februari chini ya shinikizo la Urusi na Marekani ulivunjwa mara kadhaa katika eneo la Ghouta na mikoa mingine, ingawa mashambulizi ya anga ya serikali ni madogo kuliko kabla ya kusitisha mapigano katika mkoa huo.

Miongoni mwa raia waliouwawa ni pamoja na mtoto na daktari, aliyetambuliwa kama Nabil al-Daas, aliyekuwa mtaalamu wa mwisho wa magonjwa ya wanawake katika mkoa huo, kwa mujibu wa OSDH.

Wakazi wa Ghouta waliandamana mara kadhaa kwakupinga dhidi ya mapigano baina ya waasi.

Kwa mujibu wa Abdel Rahman, mapigano yalianza wakati kundi la Faylaq al-Rahman liliendesha shambulizi dhidi ya kundi la Jaich al-Islam.

Jaich al-Islam ni kundi kubwa la waasi katika eneo la Ghouta mashariki na mmoja wa viongozi wa kisiasa, Mohammed Allouche, aliteuliwa kuwa kiongozi wa ujumbe wa kundi hili katika mazungumzo ya amani mjini Geneva, ambapo duru ya mwisho ya mwezi Aprili haikuzaa matunda yoyote.

Waasi dhidi ya serikali wamekua wakligawanyika katika makundi mengi ya kijihadi, wapiganaji wa Kiislam na waasi wenye msimamo wa wastani.

Tangu mwanzo wa vita dhidi ya utawala wa Bashar al-Assad mwezi Machi 2011, mapiganao yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 270,000 na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.