Pata taarifa kuu

Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Dunia inawatelekeza wanawake na wasichana

Kuanzia vita dhidi ya umaskini hadi kupata elimu, ikiwa ni pamoja na uwakilishi wa kisiasa au fursa za kiuchumi, dunia "haiwashirikishi wanawake na wasichana", Umoja wa Mataifa inasikitishwa katika ripoti yake kuhusu kukosekana kwa usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake iliyochapishwa siku ya Alhamisi.

Sherehe ya harusi nchini Nigeria. Wanawake huolewa kwa wastani kwa miaka 21.6, ikilinganishwa na miaka 28.5 kwa wanaume.
Sherehe ya harusi nchini Nigeria. Wanawake huolewa kwa wastani kwa miaka 21.6, ikilinganishwa na miaka 28.5 kwa wanaume. RFI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya UN Women, chombo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake inapitia Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDG) yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 na kunuiwa kujenga mustakabali bora kwa wote ifikapo mwaka 2030.

"Unapotazama takwimu, inaonyesha kwamba dunia inashindwa kusonga mbele na kufikia usawa wa kijinsia kati ya wanaume na wanawake, na hilo linazidi kuwa lengo la mbali," Sarah Hendriks, naibu mkurugenzi mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa amesema.

Mojawapo ya Maendeleo Endelevu, yanayohusu usawa wa kijinsia, yanalenga kukomesha ubaguzi, kuondoa ukatili dhidi ya wanawake, ndoa za kulazimishwa na ukeketaji, kugawana kazi za nyumbani, kuhakikisha upatikanaji wa afya ya ngono au hata kuhakikisha ushiriki mzuri katika maisha ya kisiasa na kiuchumi.

Lakini "katikati hapa njiani kuelekea mwaka 2030, dunia inawatelekeza wanawake na wasichana", na shabaha nyingi katika lengo hili mahususi haziko sawa, ripoti inabainisha.

Kila mwaka, wanawake milioni 245 wenye umri wa zaidi ya miaka 15 wanafanyiwa ukatili wa kimwili na wenzi wao, mmoja kati ya wanawake 5 ameolewa kabla ya umri wa miaka 18, wanawake hufanya kazi za nyumbani bila malipo kwa saa 2.8 kila siku. wanawakilisha 26.7% tu ya wabunge.

Ili kubadilisha hali ya mambo, dola bilioni 360 katika uwekezaji wa ziada zinahitajika kila mwaka katika takriban nchi hamsini zinazoendelea zinazowakilisha 70% ya watu duniani, shirika hilo limebaini.

Fedha ambazo "zitahimiza jumla" ya Maendeleo Endelevu (SDG), anabainisha Sarah Hendriks.

"Tunajua nini kifanyike na dunia lazima igharamie. Kama tutafanya usawa wa kijinsia kuwa lengo maalum la maendeleo, mwelekeo unaweza kubadilika," amesema, akitoa wito wa "kuwaweka wanawake na wasichana katikati".

Mnamo mwezi Julai, Umoja wa Mataifa ulikadiria kuwa Maendeleo Endelevu "yako hatarini", ukitoa "mpango wa uokoaji" wiki chache kabla ya mkutano wa kilele wa suala hili mnamo Septemba 18 na 19.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, kwa kiwango cha sasa, watu milioni 575 bado wataishi katika umaskini uliokithiri mwaka 2030, mbali na kutokomezwa kwa matumaini. Hata hivyo, milioni 342 (60%) kati yao watakuwa wanawake, au takriban mmoja kati ya wanawake kumi na wawili duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.