Pata taarifa kuu

Biden atangaza azma ya kuwania muhula wa pili wa urais Marekani

NAIROBI – Joe Biden, ametangaza Jumanne, Aprili 25, kuwa atawania muhula wa pili kama rais, katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden © AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Biden mwenye umri wa miaka 80, ametangaza azma hii mpya ya kuingia White House, akisema kila kizazi kina wakati ambapo kimelazimika kusimama kwa ajili ya demokrasia na pia kutetea uhuru wao wa kimsingi.

Naamini hii ni yetu. Ndiyo maana ninagombea kuchaguliwa tena kama rais wa Marekani. Jiunge nasi. Tumalizie kazi, Amesema Biden.

Katika miaka yake miwili ya kwanza madarakani, akikabiliwa na mapambano makubwa ya sera za kigeni, Biden hana mpinzani kutoka ndani ya Chama cha Democrat, lakini katika kampeni ambayo inaweza kusababisha marudio ya uchaguzi wa 2020 dhidi ya Donald Trump, anatarajiwa kukabiliwa na uchunguzi wa mara kwa mara na mkali juu ya umri wake, ambapo atakuwa miaka 86, atakapokuwa anamaliza muhula wake wa pili.

Rais Joe Biden katika White House, Jumatatu, Aprili 24, 2023 huko Washington.(AP Photo/Andrew Harnik)
Rais Joe Biden katika White House, Jumatatu, Aprili 24, 2023 huko Washington.(AP Photo/Andrew Harnik) AP - Andrew Harnik

Kulingana na kura ya maoni iliyofanywa na NBC News, iliyotolewa mwishoni mwa juma lililopita, iligundua kuwa asilimia 70 ya raia wa Marekani, ikiwa ni pamoja na asilimia 51 ya wanachama wa Democrat, wanaamini kwamba Biden hapaswi kugombea.

Asilimia 69 ya waliohojiwa ambao walisema hapaswi kugombea walitaja maswala juu ya umri wake kuwa sababu kubwa au ndogo ya kumtaka asigombee.

Wafuasi wake wanasema utendaji mzuri wa Chama cha Democrat katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa 2022 uliidhinisha azma ya Biden.

Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu ujao, rais Biden atakuwa na faida zote za madaraka, kwa kupata uungwaji mkono wa chama kilichoungana, wakati huu Republican wakiwa katika harakati za kumtangaza mgombea wao.

Trump, licha ya kuwa rais wa kwanza wa zamani au anayehudumu kufunguliwa mashitaka ya jinai ndiye mtangulizi mkubwa wa chama cha Republican, katika uchaguzi huu ujao.

Rais wa Marekani Donald Trump akiwa Palm Beach, Florida, Marekani, Aprili 4, 2023.
Rais wa Marekani Donald Trump akiwa Palm Beach, Florida, Marekani, Aprili 4, 2023. © REUTERS / MARCO BELLO

Mpinzani mkubwa zaidi wa chama cha Republican kwa Trump mwenye umri wa miaka 76, Gavana wa Florida Ron DeSantis, anawakilisha takwimu sawa za mrengo wa kulia, ingawa ni mdogo sana akiwa na miaka 44.

Kujenga upya tabaka la kati

Siku ya Jumanne atakapokutana na Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol, ambaye anaanza ziara yake rasmi ya kikazi ya White House, Biden atasisitiza masuala ya sera zake za kigeni.

Baadaye hivi leo Biden, anatarajiwa kutoa hotuba ya kiuchumi kwa mkutano wa muungano unaofanyika Washington, na licha ya kwamba huu sio mkutano wa kisiasa, ujumbe utakuwa jinsi ajenda yake ya kuwekeza nchini Marekani, inarudisha utengenezaji, kujenga tena tabaka la kati, na kuunda kazi za umoja zinazolipa vizuri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.