Pata taarifa kuu
WHO

WHO: Asilimia 90 ya watu duniani wanapumua hewa chafu

Ripoti ya hivi punde ya Shirika la afya duniani WHO, inaeleza kuwa watu 9 kati ya 10 wanapumua hewa chafu kote duniani.

Hewa chafu inayozalishwa kutoka viwanda mbalimbali
Hewa chafu inayozalishwa kutoka viwanda mbalimbali WHO
Matangazo ya kibiashara

WHO sasa inataka dunia kuweka mikakati ya kupambana na uchafuzi wa hewa.

Hali hii inasababisha binadamu kuambukizwa magonjwa mbalimbali na hivyo zaidi ya watu Milioni 6 kupoteza maisha.

Maria Neira Mkuu wa kitengo cha WHO kinachoshughulikia afya ya umma na Mazingira amesema, watu wanaoishi mijini ndio wanaothiriwa zaidi na kuwepo kwa hewa chafu.

Hata hivyo, watalaam wa WHO wanasema hali hii ni mbaya zaidi vijijini kinyume na inavyodhaniwa na wengi.

Aidha, ripoti hii inaeleza kuwa nchi masikini duniani ndizo zinazoathiriwa zaidi zikilinganishwa na zile zilizoendelea.

Kutokana na hali hii, WHO inasema afya ya binadamu ipo hatarini.

Ripoti hii imetolewa baada ya WHO kufanya utafiti katika maeneo 3,000 kote duniani.

Mataifa ya Kusini Mashariki mwa Asia ndio yaliyoathiriwa zaidi hasa nchini China, Malaysia na Vietnam.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.