Pata taarifa kuu
EU-TUME YA ULAYA

EU: Barroso atetea uongozi wake

Mkuu wa tume ya Ulaya inayomaliza muda wake, José Manuel Barroso ametetea leo Jumanne Oktoba 21 mbele ya mkutano mkuu wa Bunge la Ulaya mjini Strasbourg namna alivyohudumu katika mihula yake miwili kwenye uongozi wa taasisi hiyo.

José Manuel Barroso, mkuu wa tume inayomaliza muda wake,  akitetea mbele ya mkutano mkuu wa Bunge la Ulaya mjini Strasbourg namna alivyohudumu katika mihula yake miwili kwenye uongozi wa taasisi hiyo, Oktoba 21 mwak 2014.
José Manuel Barroso, mkuu wa tume inayomaliza muda wake, akitetea mbele ya mkutano mkuu wa Bunge la Ulaya mjini Strasbourg namna alivyohudumu katika mihula yake miwili kwenye uongozi wa taasisi hiyo, Oktoba 21 mwak 2014. REUTERS/Christian Hartmann
Matangazo ya kibiashara

Nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa Waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Juncker.

Akitetea kazi aliyoifanya akiwa mkuu wa tume ya Ulaya, José Manuel Barroso amesema moja ya kazi kubwa aliyoifanya ni kupanua wigo wa Umoja wa Ulaya na maendeleo yaliyopatikana katika mikataba mbalimbali. Ameonesha pia jukumu la tume ya Ulaya katika nyanja ya kimataifa, hususan misaada ya maendeleo iliyotolewa pamoja na jitihada ziliyochukuliwa kuhusu tabia nchi.

José Manuel Barroso amepongeza uwezo wa Umoja wa Ulaya wa kukabiliana na mdororo wa kiuchumi uliyojitokeza katika bara hilo, na kuanzisha utaratibu wa kiuchumi na kifedha, uliyopelekea mdororo huo kupatiwa ufumbuzi.

"Timu ambayo nilishirikiana nayo nikiwa mkuu wa tume ya Ulaya iliendesha kazi yake kwa ujasiri mkubwa, ikiweka mbele maslahi ya ya bara la Ulaya. Ni ujumbe ambao ningependa kutoa kwa kupongeza tabaka mbalimbali za watu wanaunda bara la Ulaya kwa kujitolea maendelea ya bara lao”, amesema José Manuel Barroso.

Hata hivo José Manuel Barroso, amekosolewa vikali kutokana na siasa za sera kali zilizowekwa kwa wanachama wa Umoja wa Ulaya pamoja na pesa ziliyotengwa kwa minajili ya kupiga vita umasikini na mshikamano wa kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.