Pata taarifa kuu
Brazili

Maelfu ya Raia wa Brazili waendelea na Maandamano

Maelfu ya wananchi wa Brazil wanaendelea na maandamano yao wakishinikiza kupunguzwa kwa gharama za maisha kipindi hiki ambacho kifo cha kwanza kikiripotiwa katika Mji wa Sao Paulo. 

Waandamanaji wakiwa mitaani nchini Brazil
Waandamanaji wakiwa mitaani nchini Brazil Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Polisi nchini Brazil limethibitisha mtu mmoja kupoteza maisha baada ya kugongwa na pikipiki kwenye maandamano hayo kipindi hiki wananchi wakijiapiza kuendelea kuishinikiza Serikali kutekeleza matakwa yao ya kupunguza gharama za maisha.

Haya yanakuja kipindi hiki ambacho Jeshi la Polisi likiendelea kupambana na waandamanaji wakitumia mabomu ya machozi, risasi za mpira sanjari na maji ya kuwasha ili kuwaondoa katika Mitaa ya Sao Paulo na Rio De Janeiro.

Watu wapatao milioni moja wamejitokeza kwenye maandamano hayo ya nchi nzimalicha ya Serikali ya Brazil kutangaza kupunguza gharama za usafiri ambazo zilikuwa chanzo cha kuzuka kwa maandamao hayo.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff ameahirisha ziara yake ya nje ya nchi na kuitisha Mkutano wa dharura wa Baraza la Mawaziri kuangalia njia ambazo zinaweza zikatumika kumaliza maandamano yanayohatarisha mashindano ya Mabara yanayoendelea nchini humo.

Maandamano yaliyoshika kalsi nchini Brazil ambayo yamesababisha kuwepo kwa Vurugu yametokea wakati huu Taifa hilo linapohodhi Michuano ya Kombe la Mabara.

Raia wa Brazili wanaghadhabu juu ya Maandalizi ya Michuano ya Kombe la dunia na Mashindano ya Olympiki ya mwaka 2016 wanayodai kuwa Ghali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.