Pata taarifa kuu
Zimbabwe

Zimbabwe yasema ina fedha za kutosha kuendesha zoezi la kura ya Maoni

Serikali ya Zimbabwe imesema kuwa ina fungu la fedha la kutosha kwa ajili ya gharama za kura ya maoni ili kupata katiba mpya tarehe 16 mwezi March.

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe
Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Sheria Patrick Chinamasa amesema kuwa kura hizo zitapigwa majuma matatatu yajayo hazitasitishwa kutokana na upungufu wa fedha.
 

Chinamasa amesema kuwa fedha hizo lzimepatikana kutokana na mapato ya kibiashara nchini humo.
 

Tume ya uchaguzi nchini Zimbabwe imesema inahitaji dola za kimarekani, milioni 85 kwa ajili ya zoezi la kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika baadae mwaka huu.

Uchaguzi huo unatarajiwa kumaliza serikali ya mseto nchini humo kati ya Rais Robert mugabe na Morgan Tsvangirai.

Kura za urais na ubunge zinatarajiwa kufanyika mwezi Julai, lakini kwa wakati huu kuelekea kura ya maoni, Makundi ya kutetea haki za Binaadam yametoa wito wa kuahirishwa kwa zoezi la kupiga kura za maoni kwa kile kilichoelezwa kutoa muda zaidi kwa Raia kupitia Rasimu ya katiba kwanza ili kutoa majibu ya uhakika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.