Pata taarifa kuu
Ufaransa

hatua ya kuvamia Mali yasubiri Baraka za Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, UN

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa ameeleza kuwa hatua ya kuvamia Mali ni suala linalotarajiwa kutekelezwa, akitahadharisha kuwa Maandalizi ya kupeleka vikosi 3,000 kutoka Afrika yanaendelea.

Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean- Yves Le Drian
Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa, Jean- Yves Le Drian REUTERS/Francois Lenoir
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na Radio France International Jean-Yves le Drian juma lililopita alisema uamuzi wa kutumia Jeshi umekuja kwa dhamira ya kuondoa Makundi ya kiislam yanayodhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali hivyo utafanyika baada ya Majuma kadhaa na si miezi.
 

Lakini wakati huu waziri huyu ameonekana kupingana na Kauli au matarajio yake akisema kuwa hivi sasa si wakati wa kutekeleza mpango huo ,akisema kuwa hivi sasa ni muda wa kufanya Maandalizi yanayotakiwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
 

Le Drian amesema kuwa Mataifa ya Afrika wanashughulikia mpango wa utekelezaji ambao watawasilisha katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ndani ya Mwezi mmoja na baada ya hapo swala la kuvamia Mali litajadiliwa.
 

Ufaransa imekuwa mstari wa mbele kushinikiza kuanza Operesheni dhidi ya Makundi ya kiislamu yenye Msimamo Mkali nchini Mali, ambapo Makundi hayo yanawashikilia Mateka sita Raia wa Ufaransa.
 

Ufaransa imeahidi kutoa Msaada wa Mafunzo ya Vikosi na kuwapa Vifaa mbalimbali lakini halitapeleka Jeshi lake nchini Mali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.