Pata taarifa kuu
Afghanistani

Shirika la haki za Binadamu la human Right Watch lasema wanawake wengi wapo jela nchini Afghanistani

Shirika linalotetea maswala ya haki za Binaadam, Human Rights Watch, limesema kuwa mamia ya wanawake nchini Afghanistan wanasota jela kwa makosa yanayoelezwa kuwa ukiukwaji wa maadili, ikiwemo kukimbia nyumba zao na kujihusisha na Ngono nje ya ndoa zao.

Wanawake nchini Afghanistani
Wanawake nchini Afghanistani
Matangazo ya kibiashara

Ripoti iliyotolewa mjini Kabul imetaka kuachwa huru kwa wanawake huku ripoti hiyo ikishusha shutuma kwa serikali ya Hamid Karzai kuwa imeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kusimamia sheria za kimataifa za haki za binaadam.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo Kenneth Roth amesema kuwa ni hali ya kushtusha miaka kumi baada ya mapambano na Taliban wanawake na wasichana wangali jela kwa kosa la kukimbia unyanyasaji majumbani au kulazimishwa kuozeshwa.

Wafungwa kadhaa wamehojiwa wakieleza kuwa na hofu ya kuuawa na Familia zao ili kulinda heshima ya familia hizo endapo wataachwa huru.

Kesi za wanawake na wasichana zimekuwa zikitolewa hukumu pasi na utetezi wa wanasheria na mashtaka kutosomwa mbele ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika. Wanawake hao wamekuwa wakiadhibiwa kifungo cha miaka mingi na katika kesi nyingine kifungo cha zaidi ya miaka kumi.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.