Pata taarifa kuu
Korea Kaskazini-Nyuklia

Viongozi wa nchi 53 wakutana jijini Seoul kujadili swala la Nyuklia

Rais wa Marekani Barack Obama amesema anaunga mkono sera ya ulimwengu usiokuwa na silaha za nyuklia na ameungana katika harakati za kuzuia kuenea kwa silaha hizo za nyuklia katika mkutano wa nchi 53 zinazokutana jijini Seoul nchini Korea Kusini

Barack Obama akitowa hutuba katika chuo kikuu cha Hankuk Machi 26. 2012
Barack Obama akitowa hutuba katika chuo kikuu cha Hankuk Machi 26. 2012 REUTERS/Larry Downing
Matangazo ya kibiashara

Hatari ya ugaidi wa Nyuklia imekuwa kitisho kikubwa cha usalama wa dunia ndio mana tunatakiwa kuliangalia hilo katika mkutano wa seoul, amesema rais Obama hayo rais Obama kabla ya mkutano wa kilele unaoelenga kupunguza upatikanaji wa nyuklia na makundi ya kigaidi yanaweza kutumia kama nyenzo ya mionzi na kujenga bomu ya nyuklia .

Obama pia amehakikisha kwamba Marekani inaweza kupunguza zaidi ya silaha zake za nyuklia zilizopo katika hifadhi zake.

Akizungumza katika chuo kikuu cha Hankuk Obama alielezea dhamira ya Marekani ya kupunguza zana zake za nyuklia kama taifa pekee ambalo halijwahi kutumia silaha za nyuklia.

Obama aliwaambia wanafunzi kuwa anayo imani kwamba Marekani na Russia zinaweza kwa pamoja kupunguza hifadhi yao ya silaha za nyuklia, huku zikijenga mafanikio ya makubaliano ya kudhibiti silaha unaojulikana kama START.

Ikulu ya Marekani imetangaza kuwa swala la kupunguza silaha za nyuklia linaendelea kupewa kipaumbele katika uhusiano wa Marekani na Russia, na kwamba Rais Obama ataligusia swala hilo na Rais mteule Vladimir Putin watapokutana mwezi Mei.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.