Pata taarifa kuu
Cuba-Vaticani

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Benoit XVI awasili nchini Cuba

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Baba Benoit XVI, amehitimisha ziara yake nchini Mexico asubuhi hii machi 26, 2012 na amepokekelewa kwenye uwanja wa ndege wa Santiago nchini Cuba na Raul Castro rais wa Cuba. Baadae mchana atadiriki misa ya kuadhimisha miaka 400 ya kugunduliwa kwa Bikira wa Upendo wa shaba, tajiri wa Cuba. Miaka 14 baada ya papa Jean Paul II, Benoit wa 16 ankuja kuunga mkono imani ya wananchi wa Cuba. Takriban wapinzani 70 wametiwa nguvuni jana na viongozi wa Cuba wakiwazuiz kukutana na baba Benoit XVI.

Sanamu la baba mtakatifu Benoit XVI jijini Havana
Sanamu la baba mtakatifu Benoit XVI jijini Havana Reuters/Jorge Silva
Matangazo ya kibiashara

“inabidi Cuba ifunguke kwenye ulimwengu, na ulimwengu ufunguke kwa Cuba” hayo ni matamshi ya baba mtakatifu Jean paul II wakati alipotembelea cuba mwaka 1998, matamshi ambayo hadi sasa yanakumbukwa

Hata hivyo hakuna kilichotokea ukitofautisha na nchi za mashariki. Utawala wa Fidel Castro uliendelea kumudu hali ya mambo licha ya kukabiliwa na matatizo ya kicuhumi hasa baada ya kuvunjwa kwa Umoja wa wa Sovieti. Miaka 14 baadae ni mdogo wa Fidel Castro, rais Raul Castro ndie ambae anampokea baba Benoit XVI.

Kwa serikali hiyo iliotupiliwa katika nyanja ya kimataifa, ziara ya papa ni chanya kwa ajili ya picha yake na wakati huo huo inaukumbusga ulimwengu kuwepo kwa vikwazo vya Marekani, vikwazo ambavyo vinaendelea kuathiri uchumi tangu miongo kadhaa.

Kuja kwa baba Benoit XVI kunawapa nguvu Wakatoliki waliopata uhuru wa dini katika kipindi cha miaka kumi na tano iliopita. Lakini hasa kuja kwake Cuba kunawapa matumaini ya mabadiliko. Na hayo licha ya mafunzo ya kihistoria.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.