Pata taarifa kuu
SYRIA-UN

Wajumbe wa Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura kuunga mkono juhudi za Koffi Annan nchini Syria

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon anasema mauji dhidi ya wapinzani yanayoendelea nchini Syria hayakubaliki na anatoa wito kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuungana ili kumaliza mauji hayo.

Matangazo ya kibiashara

Wito wa Moon unakuja wakati wajumbe wa baraza hilo la usalama wanapojadili mauji yanayoendelea nchini Syria yanayotuhumiwa kufanywa na wanajeshi wa serikali dhidi ya raia wanaotaka kuondoka kwa uongozi wa rais Bashar Al Asaad.

Wajumbe wa baraza hilo wanatarajiwa kupigia kura mapendekezo ya kuunga mkono juhudi za mjumbe wa umoja wa mataifa nchini Syria Koffi Annan na kumchukulia hatua rais Bashar Al Asaad ikiwa hatatekeleza mapendekezo yanayonuiwa kumaliza machafuko nchini humo.

Mapendekezo hayo yaliwasilishwa siku ya Jumatatu na Ufaransa na wajumbe wa baraza hilo wanasema wana matumaini kuwa mapendekezo hayo yatakubalika na wajumbe wote wakiwemo kutoka Urusi na Uchina ambao wamekuwa wakipinga azimio lolote dhidi ya serikali ya rais Asaad.

Upinzani nchini Syria umetakiwa kutekeleza mapendekezo ya Koffi Annan,huku wajumbe hao wakisema ikiwa mapendekezo hayo yatakubalika katika baraza hilo, rais  Asaad atachukuliwa hatua kwa kipindi cha siku saba ikiwa hataridhia mapendkezo ya Annan.

Kwa sasa wajumbe wa umoja wa mataifa wako nchini Syria kuthathmini hali ya kibinadamu nchini humo.

Machafuko nchini Syria yanaendelea kwa mwaka mmoja sasa na Umoja wa Mataifa unasema zaidi ya watu elfu nane wameuawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.