Pata taarifa kuu
Syria

Mapigano mapya yashuhudiwa mjini Damascus,wajumbe wa umoja wa mataifa waanza kuthathmini hali ya kibinadamu

Mapigano mapya yanashuhudiwa mjini Damascus nchini Syria,kati ya wanajeshi wa serikali na wapiganaji wa upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Walioshuhudia mapigano hayo mapya wanasema,mapigano hayo yameanzia katika makaazi ya al Mezze eneo ambalo pia lina ofisi kadhaa za idara ya usalama.

Runinga ya serikali ya Syria inasema wanajeshi wa serikali wamefaulu kuwaua wapiganaji wanne.

Umoja wa mataifa unasema zaidi ya watu elfu nane wameuawa tangu maandamano ya upinzani dhidi ya rais Bashar Al Asaad yalipoanza mwaka uliopita.

Wakati hayo yakijiri,wajumbe kutoka umoja wa mataifa pamoja na wale wa muungano wa jumuiya ya kiislamu wako nchini humo kuthathmini hali ya kibinadamu katika miji 15 nchini humo ikiwemo Hama na Homs.

Wajumbe hao wameitaka serikali ya Syria kushirikiana nao wakati huu wanapofanya uthathmini huo,na wanaeleza kuwa hawaegemei upande wowote na lengo lao ni kutaka kusaidia kuleta misaada ya kibinadamu kwa wale wanaoathiriwa na machafuko hayo.

Kwingineko,wawakilishi wa kiongozi wa msuluhishi wa mgogoro huo Koffi Annan nao wamewasili mjini Damascus kufuatilia mazungumzo yaliyofanyika kati ya Annan na upinzani kwa lengo la kumaliza machafuko hayo.

Ahmad Fawzi msemaji wa Koffi Annan amesema wajumbe hao watasalia nchini Syria hadi suluhu la kudumu litakapopatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.