Pata taarifa kuu
Marekani-Afghanistan

Mtuhumiwa wa mauaji ya raia 16 nchini Afghanistan atajwa.

Marekani imemtaja mwanajeshi wake anayetuhumiwa kuwaua kwa risasi raia 16 katika jimbo la kandahar nchini Afghanistan mapema juma hili kuwa ni Sajent Robert Bales ambaye ametumikia jeshi hilo kwa miaka mitatu nchini Iraq.

worldnews.msnbc.msn.com
Matangazo ya kibiashara

Bales mwenye umri wa miaka 38 siku ya jumapili aliondoka nje ya kambi ya jeshi lake huko Kandahar nchini Afghanistan na kuvamia kijiji kimoja na kuwapiga risasi raia wanawake ,wanaume na watoto.

Hatua hiyo imeendelea kuuweka pabaya uhusiano baina ya Marekani na Afghanistan tangu mwaka 2001.

Hata hivyo jeshi la Marekani halijathibitisha rasmi jina la mtuhumiwa huyo wala kumfungulia mashitaka yoyote hadi sasa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.