Pata taarifa kuu
CHINA SYRIA

China yaitaka Syria kukomesha ghasia

Serikali ya China imetoa wito wa kumalizika kwa ghasia nchini Syria ambapo utawala wa raisi Bashar Al Assad umewasha hasira ya mataifa mbalimbali duniani baada ya kuzuia misaada kuwafikia walengwa huko Baba Amr jijini Homs.

Waandamanaji nchini Syria wakipinga utawala wa raisi Bashar Al Assad
Waandamanaji nchini Syria wakipinga utawala wa raisi Bashar Al Assad 路透社
Matangazo ya kibiashara

Wakati umwagaji damu unaendelea kuripotiwa kutoka katika maeneo mbalimbali huko syria uingereza na uturuki zimejiunga na kilio cha kimataifa kulaani serikali ya Assad kufanya uhalifu na kuzuia misafara ya msalaba mwekundu kuingia baba Amr.

China, ambayo kwa mara mbili ilijiunga na urusi kuzuia maazimio ya baraza la usalama la umoja wa mataifa dhidi ya ukandamizaji unaofanywa huko syria ambapo sasa imetoa wito kwa pande zote nchini syria kukomesha mapigano pasi na masharti yoyote.

Mataifa mbalimbali yamekuwa katika shinikizo la kumtaka raisi Bashar Al Assad kusitisha umwagaji damu nchini humo na kung'oka madarakani ili kupisha demokrasia kuchukua mkondo wake nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.