Pata taarifa kuu
Marekani

Rais Obama ataka dunia iungane kuipinga, kuitenga Iran

Rais wa Marekani Barack Obama ameitaka dunia nzima kuungana ili kukabiliana na mpango wa kurutubisha nyuklia kwani utahatarisha usalama wa eneo la Mashariki ya Kati na dunia kwa ujumla.

Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais Obama amesema kuwa Marekani itasimama imara katika suala hilo na yeye mwenyewe anakutana na viongozi wa China na Urusi ili kuwashawishi wakubaliane na vikwazo vipya dhidi ya Syria.

Amesema kuwa huu ni wakati wa dunia kuungana na kuitenga Iran na kuongeza kuwa uongozi wa Marekani utafanya mazungumzo na Urusi na China katika majuma kadhaa yajayo.

Hali ya sintofahamu kati ya Iran, Israel na Marekani imezidi kuongezeka hasa baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza kuwa kuna ushahidi wa kutosha kuwa Iran ina mpango huo wa nyuklia.

Marekani na Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kutolewa vikwazo zaidi kwa utawala wa Syria lakini Urusi na China zimekuwa zikipinga hatua hiyo kuchukuliwa.

Hata hivyo Obama amekuwa akipingwa vikali na chama cha upinzani cha Republican na kusema kuwa Obama alifanya katika uamuzi wake kushughulikia suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.