Mawaziri wa fedha wa G7 wakutana jijini Marseille kujadili mbinu za kukabiliana na madeni
Mawaziri wa fedha kutoka katika mataifa, tajiri duniani yanayofahamika kama G7 wanakuataka kwa siku mbili katika mji wa Marseille nchini Ufaransa kutafuta mbinu ya kuweza kukabiliana na madeni, pamoja na namna ya kuinua uchumi wa dunia.
Imechapishwa:
Mkurugenzi mkuu wa shirika la fedha duniani, Bi.Christine Lagarde ametoa wito kwa viongozi wa mataifa hayo kushugulikia ipasavyo,na haraka iwezekanavyo changamoto za kiuchumi zinazikali mataifa yao,ili kunusuru uchumi wa dunia.
Mkutano huu unafanyaika wakati, baadhi ya mataifa barani ulaya yakikabiliwa na hali nghumu ya kiuchumi na kulazimika kubama matumizi kama vile Ugiriki, na pia biashara katika masoko ya hisa huko ulaya inaelzwa kupungua.