Pata taarifa kuu
HONG KONG-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa wabunge waahirishwa Hong Kong

Wanaharakati wanaotetea demokrasia Hong Kong wamepata pigo jipya baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi wa wabunge wa jimbo hilo kwa mwaka mmoja kutokana na janga hatari la Covid-19.

Kiongozi wa Hong Kong, Carrie Lam.
Kiongozi wa Hong Kong, Carrie Lam. ISAAC LAWRENCE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni wanafunzi kadhaa wa chuo kikuu katika jimbo hilo walikamatwa, huku kiongozi wa wanaharakati hao akimbilia mafichoni.

Mwaka mmoja baada ya maandamano ambayo hayajawahi kutokea katika koloni hilo la zamani la Uingereza tangu kupewa mamlaka ya kujitawala mwaka 1997, serikali kuu ya China ilichukua hatua ya kulidhibiti eneo hilo na kuliweka chini ya himaya yake baada ya kuweka sheria ya usalama wa kitaifa mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.

Wapinzani wengi walibaini kwamba sheria hiyo ni msumari wa mwisho kwenye jeneza kwenye kanuni ijulikanayo kama "Nchi moja, mifumo miwili", ambayo ilitakiwa kuhakikisha hadi mwaka 2047 uhuru usiojulikana mahali pengine katika China Bara.

Upinzani unaopigania demokrasia Hong Kong, ulikuwa na mataumaini ya kushinda wingi wa viti bungeni.

Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza tangu China ilipotangaza sheria mpya ya usalama wa kitaifa, ambayo adhabu yake ni kifungo cha maisha jela. China imesema sheria hiyo itatumika dhidi ya kile ilichokitaja kuwa uchochezi, njama za kujitenga, ugaidi na uingiliaji kati wa mataifa ya kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.