Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Uchaguzi wa wabunge Togo: Uchaguzi "huru, wa haki na uwazi" kulingana na shirika la kikanda

Ujumbe wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Nchi za Sahelo-Sahara (CEN-SAD), uliohusika na kuangalia uchaguzi wa Jumatatu na wa kikanda nchini Togo, uumesema uchaguzi ulikuwa "huru, wa haki na wa uwazi", wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Lomé siku ya Jumanne.

Mpiga kura akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa wabunge huko Lomé Aprili 29, 2024, nchini Togo.
Mpiga kura akipiga kura yake katika kituo cha kupigia kura wakati wa uchaguzi wa wabunge huko Lomé Aprili 29, 2024, nchini Togo. AFP - EMILE KOUTON
Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa CEN-SAD walizungumza kuhusu "uwazi na kutokuwa na kasoro kwa chaguzi mbili za Aprili 29", wakiabaini kwamba unapaswa "kuzingatiwa kuwa huru, wa haki na wa uwazi" wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari.

Jumatatu jioni, moja ya makundi makuu ya upinzani, Dynamics for the Majority of the People (DMP, kundi la vyama vya upinzani vya kisiasa na mashirika ya kiraia) lilidai, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kuona katika siku nzima ya uchaguzi "idadi kubwa kupita kiasi ya kura katika vituo kadhaa", "kuchelewa kwa kuanza kupiga kura" na orodha za wapiga kura "hazijaonyeshwa".

Raia wa Togo walilazimika kuchagua wabunge wao na washauri wao wa kikanda, katika hali ya mvutano wa kisiasa baada ya kupitisha kwa Katiba mpya Aprili 19 ambayo itahamisha nchi kutoka utawala wa rais hadi utawala wa bunge.

Changamoto ya chaguzi hizi za wabunge ni muhimu hasa kwa kuwa kiongozi wa chama kilicho wengi katika Bunge atateuliwa moja kwa moja kuwa Rais wa Baraza, aina ya Waziri Mkuu ambaye atazingatia mamlaka yote. Nafasi ya Rais wa Jamhuri inakuwa cheo rahisi cha heshima.

Upinzani wa Togo, ambao unashutumu rasimu mpya, unaona kama njia kwa mkuu wa sasa wa nchi, Faure Gnassingbé, rais tangu mwaka 2005 baada ya baba yake ambaye alitawala nchi hiyo kwa karibu miaka 38, kusalia madarakani, bila kutangaza kikomo cha idadi ya mamlaka ya urais.

Faure Gnassingbé ndiye rais wa chama cha sasa cha wengi katika Bunge la taifa, Muungano wa Jamhuri, na kwa hivyo anaweza kuchukua jukumu hili la rais wa Baraza la Mawaziri baada ya uchaguzi.

Kufikia Jumanne adhuhuri, hakuna matokeo yalikuwa yametolewa kwa umma. Kulingana na kanuni za uchaguzi, matokeo lazima yatangazwe ndani ya siku sita baada ya kupiga kura.

Upinzani unapinga Katiba mpya, lakini majaribio yote ya kupinga mageuzi ya katiba yamepigwa marufuku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.