Pata taarifa kuu

Mali: Wanamgambo kumi wanaounga mkono serikali wauawa na wanajihadi kaskazini

Wanamgambo kumi wa muungano wa makundi yenye silaha yanayoshirikiana na utawala wa Bamako waliuawa Jumatatu na wanajihadi kaskazini mwa Mali, ambapo jeshi linapambana na makundi mbalimbali ya wanajihadi na waasi wanaotaka kujitenga, kulingana na vyanzo vya usalama vilivyowasiliana na shirikala habari la AFP.

Baada ya kutaka kuondoka kwa Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), jeshi lililo madarakani lilipata ushindi wa hali ya juu kwa kuuteka mji wa Kidal (kaskazini) mwezi wa Novemba, ngome ya makundi yanayotaka kujitenga, ambayo sasa yamedhoofika
Baada ya kutaka kuondoka kwa Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), jeshi lililo madarakani lilipata ushindi wa hali ya juu kwa kuuteka mji wa Kidal (kaskazini) mwezi wa Novemba, ngome ya makundi yanayotaka kujitenga, ambayo sasa yamedhoofika © STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Hawa ni wanajihadi ambao walishambulia ngome yetu karibu na Gao Tulipoteza wapiganaji 10," Inoussa Maïga, mwanachama wa Coordination of Movements and Patriotic Resistance Front (CM-FPR), muungano unashirikiana na vikosi vya serikali katika vita dhidi ya wanajihadi, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumanne . Shambulio hilo lilitokea siku ya Jumatatu katika mji wa Kadji, uliopo nje kidogo ya mji wa Gao, mwendo wa saa 7:30 mchana (saa za ndani), kwa mujibu wa chanzo cha polisi cha Mali kilichowasiliana na shirika la habari la AFP na waraka wa ndani wa makundi haya yenye silaha ambayo pia yanathibitisha idadi hii

Eneo la Gao ni eneo la mapigano ya mara kwa mara kati ya wanajihadi wengi kutoka jamii ya  Watuareg au makundi yanayotaka kujitenga na jeshi la Mali, likisaidiwa na washirika wake wa Urusi na makundi ya wenyeji yenye silaha. Mavuguvugu yanayohusiana na CM-FPR yanatawaliwa na wanachama wa jumuiya zisizofanya kazi, hasa Songhai, ambao wamekuwa katika migogoro kwa miongo kadhaa na wakazi wa kuhamahama wa eneo hili la nusu jangwa.

Uhaba wa malisho na maendeleo ya ardhi ya kilimo, pamoja na matukio ya ukame, umeongeza mivutano kati ya wakulima na wafugaji na kuhimiza kuibuka kwa makundi ya wahalifu na kisha kijihadi ambayo yameiingiza nchi na eneo hilo katika mzunguko wa vurugu. Wanajeshi waliochukua mamlaka mwaka 2020 waliahidi kurejesha udhibiti wa eneo lote la taifa na kuvunja ushirikiano wao wa kijeshi na Ufaransa na hivyo kusogelea Urusi.

Baada ya kutaka kuondoka kwa Misheni ya Umoja wa Mataifa nchini Mali (MINUSMA), jeshi lililo madarakani lilipata ushindi wa hali ya juu kwa kuuteka mji wa Kidal (kaskazini) mwezi wa Novemba, ngome ya makundi yanayotaka kujitenga, ambayo sasa yamedhoofika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.