Pata taarifa kuu

Mali: jeshi lamuangamiza kiongozi wa kijeshi wa kundi la Islamic State

Nchini Mali, jeshi limetangaza kumuua Abu Huzeifa. Kwa jina la utani Higgo, kiongozi huyu muhimu wa wanajihadi wa Islamic State katika Sahel (EIS) aliuawa asubuhi ya Jumapili Aprili 28, wakati wa operesheni iliyofanywa kusini mashariki mwa Indelimane, Kaskazini mwa nchi, karibu na mpaka wa Nigeria.

Jeshi la Mali katika eneo la kaskazini, mjini Goundam, karibu na mji wa Timbuktu, mwezi Juni mwaka 2015.
Jeshi la Mali katika eneo la kaskazini, mjini Goundam, karibu na mji wa Timbuktu, mwezi Juni mwaka 2015. © AFP/PHILIPPE DESMAZES
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hizo zilianza kusambaa siku ya Jumapili, lakini hazikuwa zimethibitishwa na chanzo rasmi. Kwa mujibu wa jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Wagner wa Urusi, kuuawa kwa kiongozi huyu ni mafanikio yasiyopingika.

Abu Huzeifa alikuwa kamanda wa kijeshi wa kundi la Islamic State katika Sahel, katika eneo la mpaka wa Mali-Niger-Burkina Faso. Kazi yake kuu ya kijeshi? ni ile ya kushiriki katika shambulio la Tongo Tongo mwaka 2017, nchini Niger, ambapo wanajeshi wanne wa kikosi maalum cha Marekani na wanajeshi wanne wa Niger waliuawa. Katika moja ya picha zake adimu zinazosambazwa, anapiga picha na silaha iliyoibiwa kutoka kwa askari wa Marekani wakati wa shambulio hili. Kisha Marekani kitita cha pesa kwa yeyote atakaye muua au kufanikisha kupatikana kwa kiongozi huyu wa Islami State katika Sahel, ikitoa hadi dola milioni 5 kwa taarifa zozote zitakazoelekeza mahali alipo.

Akiwa na ndevu ndefu sana, aliyepewa jina la utani Higgo au Higgo El Maghribi, Abu Huzeifa alikuwa "huenda" mwenye asili ya Sahrawi, kulingana na wataalamu kadhaa, kama vile kiongozi wake wa zamani Adnan Abou Walid al-Sahraoui, amiri wa tawi la kundi la Islamic State katika Sahelaliyeuawa mnamo Agosti 2021 na jeshi la Ufaransa.

Miaka miwili iliyopita, mwezi Machi 2022, kundi la Islamic State lilianzisha mashambulizi makubwa katika eneo la Ménaka, likiua kinyama, kulingana na makadirio ya ndani, zaidi ya watu elfu moja na kuchoma vijiji vingi. Leo, karibu eneo lote la Ménaka na sehemu ya eneo la Gao ziko chini ya udhibiti wa EIS, ambao kwa hiyo limepoteza moja ya nguzo zake katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.