Pata taarifa kuu

Makamu wa rais wa Marekani yuko nchini Tanzania kwa ziara

NAIROBI – Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris amewasili  nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi wa siku tatu akitokea nchini Ghana kabla ya kuelekea nchini Zambia kukamilisha ziara yake barani Afrika.

Kamala Harris, Makamu wa rais wa Marekani yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.
Kamala Harris, Makamu wa rais wa Marekani yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi. © REUTERS - WOLFGANG RATTAY
Matangazo ya kibiashara

Makamu huyo wa Rais amewasili majira ya saa tano za usiku katika uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Tanzania Dokta Phillip Mpango.

Leo hii atafanya Mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuhusu namna ya kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia na pamoja na Nyanja nyingine ikiwemo za Biashara na Uwekezaji, Usalama, Ubunifu na Ugunduzi.

Ziara hii ina tija gani kwa Tanzania? Dkt.Suleimani Haji Suleimani ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

“Biashara kati ya nchi zetu imekuwa, tumekuwa tukisafirisha bidhaa mbalimbali.” amesema Dkt.Suleimani Haji Suleimani ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

00:08

Suleimani Haji Suleimani

Nao raia wa nchini humo wanazungumziaje ziara hii ya Kamala Harris katika taifa hilo la Afrika Mashariki?

“Ujio wake unaleta uhusiano mzuri wa kiamataifa kati ya Tanzania na Marekani.” ameeleza mmoja wa raia nchini humo.

00:19

Maoni ya raia wa Tanzania kuhusu zaira ya Kamala Harris

Marekani imewekeza katika miradi 266 yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 4.78.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.