Pata taarifa kuu

Uingereza yatenga euro milioni 120 kulinda maeneo ya ibada

Wakati Ramadhani inaanza kwa jamii ya Waislamu duniani kote, serikali ya Uingereza inatangaza uwekezaji wa pauni milioni 117 kulinda maeneo ya ibada na vituo vya kitamaduni. Waislamu nchini Uingereza kwa sasa wanakabiliwa na ongezeko la chuki dhidi ya Uislamu.

Msikiti mkuu wa London
Msikiti mkuu wa London Asim Saleem (Asim18) / Wikimedia Commons
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa London, Émeline Vin

Zaidi ya euro milioni 120 zitatengwa kwa muda wa miaka minne ili kufunga kamera za uchunguzi, uzio unaostahimili zaidi na mifumo ya kengele katika misikiti, shule za Kiislamu na maeneo ya kitamaduni. Njia ya kulinda maeneo yanayohusiana na Uislamu na waumini kutokana na mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu.

Vitisho na matusi

Kulingana na chama ambacho hukusanya shuhuda kutoka kwa waathiriwa, mashambulizi haya yaliongezeka mara tatu kati ya mwezi Oktoba na Februari, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka mmoja mapema. Shirika lisilo la kiserikali la Tell Mama inaunganisha moja kwa moja kati ya ongezeko hili la mashambulizi na vita huko Gaza. Matukio haya yanahusisha zaidi matusi kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia vitisho vinavyorushwa misikitini na matusi mitaani. Wanawake wanawakilisha thuluthi mbili ya waathiriwa.

"Hakikisho"

Ufadhili uliotolewa leo Jumatatu Machi 11 na serikali unapaswa kufanya uwezekano wa "kuihakikishia" jamii ya Waislamu, wakati chuki dhidi ya Uislamu haina ufafanuzi rasmi katika sheria za Uingereza na naibu mkuu wa chama tawala cha Conservative alifukuzwa kazi wiki mbili zilizopita kwa kulinganisha Uislamu na itikadi kali na kukataa kuomba msamaha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.