Pata taarifa kuu
UHURU-IMANI

Ulimwengu wa Kiislamu walaani kitendo cha kuchoma moto Quran nchini Sweden

Nchi nyingi za Kiislamu siku ya Alhamisi zimeshutumu "kitendo cha chuki" na "uchochezi" baada ya mtu mmoja kuchoma kurasa za nakala ya Quran mbele ya Msikiti wa Stockholm wakati wa maandamano yaliyoidhinishwa na mamlaka ya Sweden.

Salwan Momika, Muiraq mwenye umri wa miaka 37 ambaye aliikimbia nchi yake kuelekea Sweden, alikanyaga Quran mara kadhaa kabla ya kuchoma kurasa chache nje ya Msikiti Mkuu huko Stockholm mnamo Juni 28, 2023.
Salwan Momika, Muiraq mwenye umri wa miaka 37 ambaye aliikimbia nchi yake kuelekea Sweden, alikanyaga Quran mara kadhaa kabla ya kuchoma kurasa chache nje ya Msikiti Mkuu huko Stockholm mnamo Juni 28, 2023. AFP - JONATHAN NACKSTRAND
Matangazo ya kibiashara

Raia wa Iraq ambaye aliikimbia nchi yake kuelekea Uswisi alikanyaga nakala ya Quran mbele ya Msikiti mkubwa kabisa mjini Stockholm siku ya Jumatano kabla ya kuchoma kurasa kadhaa, katika siku ya kwanza ya sikukuu kuu ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Tukio la aina hii, ambalo tayari limetokea nchini Uswisi au katika nchi zingine za Ulaya, wakati mwingine kwa mpango wa harakati za mrengo wa kulia, hapo awali lilisababisha maandamano na mivutano ya kidiplomasia.

Serikali ya Iraq imeshutumu "vitendo vya kibaguzi, kuchochea ghasia na chuki" ambavyo hutokea "mara kwa mara" katika nchi "ambazo zinajivunia kukumbatia tofauti na kuheshimu imani za wengine". Na Wizara ya Mambo ya Nje imeshutumu "ruhusa iliyotolewa na mamlaka ya Sweden kwa mtu mwenye msimamo mkali kuchoma nakala ya Quran Tukufu".

Wito wa kufanyika kwa maandamano

Kiongozi wa kidini wa Kishia mwenye ushawishi mkubwa, Moqtada Sadr, ambaye ni mtu muhimu katika siasa nchini Iraq, ametoa wito wa kufanyika maandamano mbele ya ubalozi wa Sweden mjini Baghdad kushinikiza "kutimuliwa kwa balozi" na kufuta uraia Iraq wa "mhalifu", raia wa Iraq, ambaye alichoma moto Quran huko Stockholm.

Saudi Arabia, ambako kunapatikana miji miwili mitakatifu ya Makkah na Madina, imelaani "vitendo vya chuki vinavyorudiwa mara kwa mara (...) vinavyochochea chuki, kutengwa na ubaguzi wa rangi, na kupinga juhudi za kueneza maadili ya kuvumiliana". Ufalme mwingine wa Ghuba, Kuwait, umetaka wahusika wa "vitendo vya uadui" hivyo kuhukumiwa na "kuzuiwa kutumia kanuni ya uhuru (...) kuhalalisha uadui dhidi ya Uislamu".

"Serikali na watu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (...) hawavumilii tusi kama hilo", kwa upande wake ametangaza mjini Tehran msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Nasser Kanani, akilaani kitendo "kisichokubalika". Morocco imemrejesa numbani balozi wake nchini Uswisi, ikilaani kitendo "kisicho kuwajibika" na "chokozi za mara kwa mara, zilizofanywa huku serikali ya Sweden ikishangilia".

Misri, nchi yenye watu wengi zaidi kati ya nchi za Kiarabu, imekashifu "ishara ya aibu na uchochezi kwa hisia za Waislamu" wakati huo huo wa Eid al-Adha, sikukuu kubwa ya dhabihu inayosherehekewa na Waislamu kote ulimwenguni. Nchini Syria, serikali "imeshutumu kwa maneno makali zaidi kitendo cha aibu 'kilichofanywa' na mtu mwenye msimamo mkali kwa ruhusa (...) ya serikali ya Sweden."

Huko Beirut, vuguvugu lenye nguvu la Hezbollah pia limeshutumu mamlaka ya Uswisi kuwa "mshiriki katika uhalifu", ikitoa wito kwa Stockholm kukomesha vitendo kama hivyo "badala ya kujificha nyuma ya uhuru wa kujieleza". Imetoa wito kwa nchi za Kiislamu na Kiarabu kuchukua "hatua zote zinazohitajika" kuilazimisha Sweden na nchi nyingine kuzuia kujirudia kwa matukio hayo na kukomesha "kuenea kwa utamaduni wa chuki".

'Utamaduni wa chuki'

Katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Anwar Gargash, mshauri wa kwanza wa rais, amebaini kwenye mitandao ya kijamii kwamba "ulimwengu wa Magharibi lazima utambue kwamba mfumo wake wa thamani na uhalali wake hauwezi kuwekwa kwa ulimwengu". Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina imeshutumu "ukiukaji mkubwa wa (...) maadili ya uvumilivu, kukubalika kwa wengine".

Mashirika katika eneo hilo pia yametoa hisia zao, kama vile Jumuiya ya Waarabu ambayo imelaani "uchokozi katika moyo wa imani yetu ya Kiislamu". Baraza la Ushirikiano la Ghuba (GCC) limeishushia lawama "mamlaka ya Swedenna kubaini kwamba inawajibika kwa athari zote zinazotokana na vitendo hivi", huku Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) ikilaani "vikali" kitendo hiki.

Tukio hilo pia liliamsha hasira nchini Uturuki, ambapo Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan amesema kuwa "kufumbia macho vitendo hivyo vya kinyama ni kujihusisha" kwa vitendo vya haramu. Huko Kabul, serikali ya Taliban imelaani kitendo hiki na kusema ni "dharau kabisa" kwa Uislamu.

Maandamano ya mwezi Januari ambapo nakala ya Quran ilichomwa moto huko Stockholm mbele ya ubalozi wa Uturuki yalizua hasira katika ulimwengu wa Kiislamu na maandamano na kutoa wito wa kususia bidhaa kutoka Sweden.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.