Pata taarifa kuu

Ulaya: Asilimia 40 ya raia wanafariki kutokana na matatizo ya ugonjwa wa moyo

Ugonjwa wa moyo unahusika na asilimia 40 ya vifo barani Ulaya, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la afya duniani, WHO, ambapo limewataka raia kwenye eneo hilo kupunguza ulaji wa chumvi.

Takwimu zinaonesha nchi 51 kati ya 53 katika ukanda wa Ulaya zina wastani wa ulaji wa chumvi kila siku zaidi ya kiwango kilichopendekezwa na WHO cha gramu tano.
Takwimu zinaonesha nchi 51 kati ya 53 katika ukanda wa Ulaya zina wastani wa ulaji wa chumvi kila siku zaidi ya kiwango kilichopendekezwa na WHO cha gramu tano. © Getty Images/Manusapon Kasosod
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa WHO, hii ni sawa na vifo elfu 10 kwa siku, au milioni nne kwa mwaka, shirika hilo likiongeza kuwa Utekelezaji wa sera zinazolenga kupunguza matumizi ya chumvi kwa asilimia 25 zinaweza kuokoa maisha ya takriban watu laki 9 kutokana na magonjwa ya moyo na mishipa ifikapo 2030,"

Mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya Ulaya, Hans Kluge, amesema mtu mzima mmoja kati ya watatu walio na umri wa kati ya miaka 30 na 70 wanakabiliwa na shinikizo la damu, na mara nyingi kutokana na matumizi ya chumvi.

Takwimu zinaonesha nchi 51 kati ya 53 katika ukanda wa Ulaya zina wastani wa ulaji wa chumvi kila siku zaidi ya kiwango kilichopendekezwa na WHO cha gramu tano, au kijiko kimoja cha chai.

Kulingana na ripoti ya WHO kanda ya Ulaya, wanaume katika eneo hilo wana uwezekano wa karibu mara 2 wa kufa kutokana na magonjwa ya moyo na mishipa kuliko wanawake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.