Pata taarifa kuu

Takriban wahamiaji 140 waokolewa Manche

Takriban watu140 waliokuwa kutafuta hifadhi ya ukimbizi wakijaribu kuingia nchini Uingereza kwa boti mbili zilizokuwa zikisafiri kinyime cha sheria waliokolewa siku ya Jumamosi kwenye pwani ya Ufaransa na meli mbili zilizokodishwa na serikali ya Ufaransa, mamlaka katika eneo hilo imesema siku ya Jumapili. Wengine watano waliokolewa siku ya Jumamosi baada ya meli yao kuzama, mamlaka katika eneo la Pas-de-Calais limeongeza.

Meli za vikosi vya majini vya Ufaransa na Uingereza wakati wa operesheni ya uokoaji kwenye pwani ya Calais kwenye eneo la Manche, mnamo Agosti 2023.
Meli za vikosi vya majini vya Ufaransa na Uingereza wakati wa operesheni ya uokoaji kwenye pwani ya Calais kwenye eneo la Manche, mnamo Agosti 2023. AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

 

Kulingana na mamlaka ya eneo la Manche na eneo la Bahari ya Kaskazini (Prémar), mamlaka kwanza iliokoa siku ya Jumamosi asubuhi wahamiaji 57 ambao walikuwa wameingia baharini karibu na Gravelines (kaskazini) Jumamosi usiku, baada ya meli yao kupata tatizo.

Wakiokolewa na Ridens, meli inayoshiriki katika mfumo wa ufuatiliaji na uokoaji ulioanzishwa na mamalaka katika Mlango wa Bahari wa Pas-de-Calais, wasafiri hao "walishushwa na kutunzwa na huduma za dharura kwenye nchi kavu" kwenye bandari ya Calais, inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Premar.

Katikati ya mchana, watu 75 waliokuwa kwenye boti wakiomba usaidizi pia waliokolewa na kurejeshwa na meli ya usaidizi na uokoaji Abeille Normandie hadi nchi kavu. "Walishushwa kwenye bandari ya Boulogne-sur-Mer mbele ya timu za uokoaji," taarifa kwa vyombo vya habari inabaini.

Aidha, watu watano, akiwemo mtoto mchanga wa miezi minne, waliokolewa baada ya meli yao kzama karibu na Boulogne-sur-Mer (kaskazini), mamlaka ya mkoa wa Pas-de-Calais imeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumamosi. Kulingana na Gazeti la La Voix du Nord, watu hawa wote wanatoka katika familia moja ya Wakurdi.

Takriban wahamiaji 36,000 walijaribu kuingia Uingereza mwaka 2023 kwa kuvuka Manche kinyume cha sheria kutoka pwani ya Ufaransa, idadi iliyopungua kwa zaidi ya 30% kwa mwaka mmoja, kulingana na ripoti iliyowasilishwa mwanzoni mwa mwezi wa Februari na mamlaka ya eneo hilo, ambayo inataja vifo 12 kwa mwaka mmoja uliopita.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.