Pata taarifa kuu

Meli ya wahamiaji iliyozama Manche: askari watano wa Ufaransa washtakiwa

Uchunguzi wa tukio la kuzama kwa boti lililosababisha vifo vya wahamiaji 27 baharini katika eneo la Manche mnamo Novemba 2021, unazidi kushika kasi kwa kufunguliwa mashitaka Alhamisi, Mei 25 kwa askari watano, wanaoshukiwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.

Mtumbwi ulioharibika na gunia la kulalia lililotelekezwa na wahamiaji kwenye ufuo karibu na Wimereux, Ufaransa. Takriban wahamiaji 31 ​​walizama katika wakisafiri na bolti lao kutoka Calais siku ya Jumatano walipokuwa wanataka kufika Uingereza, ajali iliyoelezwa kuwa "janga" na serikali ya Ufaransa ambayo ilitangaza kukamatwa kwa watu wanne kwa madai ya kuhusika kwao.
Mtumbwi ulioharibika na gunia la kulalia lililotelekezwa na wahamiaji kwenye ufuo karibu na Wimereux, Ufaransa. Takriban wahamiaji 31 ​​walizama katika wakisafiri na bolti lao kutoka Calais siku ya Jumatano walipokuwa wanataka kufika Uingereza, ajali iliyoelezwa kuwa "janga" na serikali ya Ufaransa ambayo ilitangaza kukamatwa kwa watu wanne kwa madai ya kuhusika kwao. © REUTERS/Gonzalo Fuentes
Matangazo ya kibiashara

Watu tisa, wakiwemo askari wasiopungua watano kutoka Kituo cha Gris-Nez (Cross, Pas-de-Calais), walikuwa wametiwa mbaroni katika siku za hivi karibuni na kuhojiwa na idara ya Utafiti ya polisi inayohusika na masuala ya safari za baharini ya Cherbourg, kulingana. na chanzo cha mahakama na chanzo kinachofahamu suala hilo.

Wanajeshi hawa watano, wanawake watatu na wanaume wawili, walionyeshwa siku ya Alhamisi, Mei 25 alasiri kwa mahakimu wapelelezi wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mapambano dhidi ya Uhalifu uliopangwa (Junalco) kutoka Mahakama ya Haki ya Paris. Kulingana na chanzo cha mahakama, walishtakiwa kwa kushindwa kumsaidia mtu aliye hatarini na kuachwa huru baada ya kuhojiwa. Kanuni ya sheria ya kijeshi inazuia kwa nguvu uwezekano wa kuwaweka askari chini ya usimamizi wa mahakama.

Uchunguzi unaendelea, lakini hautoshi kwa Charlotte Kwantes, mratibu wa kitaifa wa Utopia 56. "Tunajaribu kutoa mwanga juu ya wajibu wa serikali ya Ufaransa na Uingereza katika janga hili," amebaini. "Mbali na jukumu la kibinafsi la maafisa wanaotakiwa kutekeleza sheria, tutaendelea kutafuta jukumu la Serikali katika tamthilia hii na katika hali ya kuwajali watu wanaojaribu kuvuka Manche. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.