Pata taarifa kuu

Vita Ukraine: Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kuzuru Kyiv

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa mjini Kyiv Jumapili hii, taarifa ambazo hazijathibitishwa kwa upande wa Marekani.

Mwanajeshi wa kike wa Ukraine katika kituo cha ukaguzi huko Bakhmut, mashariki mwa Ukraine, Aprili 23, 2022.
Mwanajeshi wa kike wa Ukraine katika kituo cha ukaguzi huko Bakhmut, mashariki mwa Ukraine, Aprili 23, 2022. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Ikiwa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi itafanyika, itakuwa ziara ya kwanza rasmi ya wajumbe wa utawala wa Biden tangu kuanza kwa vita hivi vya Urusi dhidi ya Ukraine, anaelezea mwandishi wetu wa New York, Loubna Anaki. Na hiyo labda haitaifurahisha Urusi.

Itafahamika kwamba kwa miezi miwili, Marekani imetuma msaada wa karibu dola bilioni tatu na nusu kwa Ukraine. Na siku chache tu zilizopita, Ikulu ya Marekani iliidhinisha kutumwa kwa misaada ya kijeshi ikiwa ni pamoja na vifaa muhimu vya jeshi ikilinganishwa na vile ambavyo vimetumwa hadi sasa - ndege zisizo na rubani, mifumo ya ulinzi ya rada.

Misaada ambayo hivi karibuni Marekani ilipata onyo kutoka kwa Urusi. Moscow ilikuwa imeonya juu ya "matokeo yasiyotarajiwa ikiwa Washington itaendelea kusambaza silaha". Ikiwa Antony Blinken na Loyd Austin wanakwenda Kyiv, huu utakuwa ujumbe ulio wazi kwa Moscow: Marekani Itaendelea kuunga mkono Ukraine.

Kwa kutangaza ziara hii, Volodymyr Zelensky pia amesema anatumai Joe Biden atakuja mara tu hali ya usalama itakaporuhusu. Rais wa Ukraine pia amemkosoa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ambaye pia anatarajiwa nchini Ukraine na Urusi. Alisema anasikitishwa kuaona Antonio Guterres anaanzia zaia Moscow.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres atafanya ziara hadi Urusi Jumanne tarehe 26 Aprili ambapo atapokelewa na Vladimir Putin. Hii ni mara ya kwanza kwa afisa huyo wa Umoja wa Mataifa kupokelewa na mamlaka ya Urusi tangu kuanza kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine tarehe 24 Februari.

Katika hatua nyingine, idadi ya wakimbizi wanaokimbia uvamizi wa Urusi inakaribia milioni 5.2, kulingana na Umoja wa Mataifa. Zaidi ya watu milioni 7.7 wamehama nyumba zao lakini bado wako Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.