Pata taarifa kuu

Ukraine: Moldova yatiwa wasiwasi kuhusu malengo ya Urusi na yamwitisha balozi wa Urusi

Katika siku ya 58 ya uvamizi wa Kirusi wa Ukraine, hatima ya bandari ya kimkakati ya Mariupol, ambayo Moscow inadai kuwa "imekomboa", bado haijulikani. Kyiv inasema watu wake bado wanapigana na vikosi vya Urusi katika kiwanda kikubwa cha madini cha Azovstal. Vladimir Putin amehakikisha kwa upande wake kwamba Ukraine inawazuia wanajeshi wake kujisalimisha.

Bendera ya Moldova huko Chisinau.
Bendera ya Moldova huko Chisinau. © Parlamentul Republicii Moldova - Public Domain
Matangazo ya kibiashara

Katika siku ya 58 ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hatima ya bandari ya kimkakati ya Mariupol, ambayo Moscow inadai kuwa "imekomboa", bado haijulikani. Kyiv inasema watu wake bado wanapigana na vikosi vya Urusi katika kiwanda kikubwa cha madini katika eneo la Azovstal huko Mariupol.

"Moja ya malengo ya jeshi la Urusi ni kuweka udhibiti kamili katika mji wa Donbass na kusini mwa Ukraine", afisa mkuu wa jeshi la Urusi alisema Ijumaa, akizungumzia "awamu ya pili ya operesheni maalum" inayolenga, pamoja na mambo mengine, " kuhakikisha kumekuwa na eneosalama la kiutu kuelekea Crimea."

Bandari ya kimkakati ya Mariupol, ambayo Moscow inadai "imekomboa", bado wanajeshi wa Ukraine wanapigana na vikosi vya Urusi, inasema Kyiv, ambayo inabaini kwamba wapiganaji wa wa Ukraine wanaendelea kutetea vikali kiwanda kikubwa cha chuma huko Azovstal, ambapo raia pia wamekimbilia.

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel amemwomba Rais wa Urusi Vladimir Putin leo Ijumaa ahakikishe kuna kuwa na maeneo ya usalama wa kiutu huko Mariupol wakati wa Pasaka ya Kiorthodoksi. Naibu Waziri Mkuu wa Ukraine Iryna Vereshchuk alitangaza kuwa hakuna maeneo ya usalama wa kiutu yatakayowekwa Ijumaa hii, hali ikiwa ni "hatari" sana barabarani.

Umoja wa Mataifa umeshutumu jeshi la Urusi kwa vitendo ambavyo "vinaweza kuwa uhalifu wa kivita" nchini Ukraine. Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wameandika "mauaji, ikiwa ni pamoja na mauaji ya kiholela" ya raia 50 katika mji wa Bucha, nje kidogo ya mji wa Kyiv, ambapo vikosi vya Urusi vinashutumiwa kufanya mauaji yaliosababisha vifo vya makumi ya watu. Madai ambayo Moscow inakanusha.

Mazungumzo kati ya Moscow na Kyiv kutafuta suluhisho la mzozo huo "yameshindwa", waziri wa mambo ya nje wa Urusi alisema Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.