Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Idadi ya wagonjwa yapungua Ufaransa, idadi ya vifo yaongezeka

Janga la Covid-19 bado linaendelea ulimwenguni, huku idadi ya maambukizi ikivuka watu milioni 2. Nchini Ufaransa, idadi ya wagonjwa wa Covid-19 imepunguwa kwa mara ya kwanza, lakini bado iko kwenye kiwango cha juu.

Nchini Ufaransa, kulingana na ripoti ya mwisho kutoka Wizara ya Afya Jumatano jioni, Aprili 15, kesi 106,206 za maambukizi ya Covid-19 zimethibitishwa pamoja na vifo vya watu 17,167 nchini.
Nchini Ufaransa, kulingana na ripoti ya mwisho kutoka Wizara ya Afya Jumatano jioni, Aprili 15, kesi 106,206 za maambukizi ya Covid-19 zimethibitishwa pamoja na vifo vya watu 17,167 nchini. REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo janga la Covid-19 limeanza kutoweka katika mkoa wa PACA.

Ugonjwa wa Covid-19 unaendelea kuenea ulimwenguni: nchi 185 zimeathiriwa na ugonjwa huo, zaidi ya watu milioni 2 wameambukizwa virusi vya Corona na zaidi ya watu 128,000 wamefariki dunia. Kufikia sasa, watu 465,000 wameponya ugonjwa wa Covid-19.

Marekani ni nchi ambayo imeathiriwa zaidi, ikiwa na wagonjwa zaidi ya 610,000 na vifo 26,000. Inafuata Italia ambapo watu 21,000 wamefariki dunia na Uhispania ambapo watu 18,500 wamefariki dunia, Profesa Jérôme Salomon, Mkurugenzi mkuu wa Afya nchini Ufaransa alisema.

Nchini Ufaransa, kulingana na ripoti ya mwisho kutoka Wizara ya Afya Jumatano jioni, Aprili 15, kesi 106,206 za maambukizi ya Covid-19 zimethibitishwa pamoja na vifo vya watu 17,167 nchini.

Watu 31,779 bado wamelazwa hospitalini kwa maambukizi ya COVID-19, licha ya kupungua kwa wagonjwa wachache 513 kuliko siku iliyopita.

"Wanasayansi wanakadiria kuwa karibu 10% ya raia wa Ufaransa tayari wameambukizwa virusi hivyo," Waziri wa Afya wa Ufaransa, Olivier Véran, alitangaza Jumatatu Aprili 13 kwenye kituo cha redio ya RTL.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.