Pata taarifa kuu
UFARANSA-CORONA-AFYA

Ufaransa kuendelea na hatua za tahadhari hadi Mei 11

Rais wa Ufaransa amelihutubia taifa Jumatatu jioni kwa mara ya nne tangu kuanza kwa mgogoro wa kiafya uliotokana na janga la kimataifa la Covid-19.

Emmanuel Macron, Jumatatu Aprili 13, alitangaza kuongeza muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maamukizi ya virusi vya corona hadi Mei 1.
Emmanuel Macron, Jumatatu Aprili 13, alitangaza kuongeza muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maamukizi ya virusi vya corona hadi Mei 1. Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Rais amebaini kwamba "ugonjwa huo umeanza kupungua" nchini Ufaransa na kutangaza kuongeza muda wa kuendelea kuchukua tahadhari za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona hadi Mei 11.

Ugonjwa wa Covid-19 umeuwa watu 14,967 nchini Ufaransa, huku wengine wakiendelea kuhudumiwa katika hospitali mbalimbali.

Akielezea kwa undani jinsi serikali inavyokabiliana na mgogoro wa kiafya kutokana na ugonjwa huo na jinsi inakusudia kuutokomeza nchini, rais wa Ufaransa amezungumzia kuhusu mambo kadhaa.

Muda wa kuendelea kubaki nyumbani waongezwa

Licha ya janga hilo ambalo "limeanza kupungua", rais wa Ufaransa ametangaza kwamba "hatua za tahadhari za kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona zitaendelea hadi Mei 11."

Ifikapo Mei 11, shule za chekechea, shule za msingi, shule za sekondari na vyuo vikuu vitaanza shughulizao. Hata hivyo, sheria maalum zitawekwa. Kuhusu elimu ya juu, shughuli zitaanza tena "rasmi" kabla ya msimu wa joto. Maeneo wanako kusanyika watu wengi, ikiwa ni pamoja na baa, mikahawa, hoteli au majumba ya kumbukumbu, zitaendelea kufungwa, ametangaza rais Emmanuel Macron. Hakutakuwa na sherehe "kabla ya katikati ya mwezi wa Julai".

Idadi ya wagonjwa wa COVID-19 wanaohitaji uangalizi maalumu imepungua kwa siku ya tano mfululizo. Macron amesema kasi ya janga hilo inaanza kupungua na dalili za kudhihirisha hilo ziko wazi. "Mei 11 itakuwa mwanzo wa awamu mpya. Sheria zinaweza kubadilishwa kulingana na hali itakavyokuwa," aliongeza Macron.

Tangazo hilo la Macron limetolewa baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kusema kwamba kuondoa vizuizi vilivyowekwa mapema sana kunaweza kuleta wimbi la pili la maambukizi, na kuonya kuwa chanjo tu ndio itazuia kabisa kuenea kwa ugonjwa wa COVID-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.