Pata taarifa kuu
UFARANSA-AFRIKA-CORONA-UCHUMI

Coronavirus: Emmanuel Macron atoa wito wa 'kufutwa' kwa madeni ya nchi za Afrika

Ufaransa na Ulaya wanatarajia kusaidia Afrika kupambana dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 kwa "kuifutia kabisa madeni yake," Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema Jumatatu katika hotuba kwa taifa.

Rais wa Ufaransa wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kwa mabalozi wa Ufaransa (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Ufaransa wakati wa hotuba yake ya kila mwaka kwa mabalozi wa Ufaransa (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Philippe Wojazer/Pool
Matangazo ya kibiashara

Rais Macron ameungana na baadhi ya viongozi duniani kutoa wito huo.

Jumatatu jioni, Emmanuel Macron amesikika akiunga mkono ombi lililotolewa hivi karibuni na viongozi kadhaa wa Afrika, ikiwa ni pamoja na rais wa Senegal Macky Sall, na kiongozi wa kanisa Katolika Papa Francis siku ya Jumapili.

Wito huo unakuja baada ya taasisi kadhaa za fedha za kimataifa kama vile IMF na Benki ya Dunia kutoa wito kwa nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda kusamehe madani kwa nchi za Afrika katika kuzisaidia kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19. Ugonjwa huu ambao Umoja wa Mataifa uliutaka kuwa ni janga la kimataifa umeendelea kuwa tishio kubwa ulimwenguni hasa barani Afrika, ambapo nchini nyingi ni masikini, huku raia wao wakiishi katika mazingira magumu.

Suala hilo linatarajiwa kujadiliwa wiki hii na nchi zilizostawi kiuchumi na kiviwanda, G20, kando ya mkutano wa Shirika la Fedha la Kimataifa.

Tangu wiki tatu zilizopita viongozi wa nchi zenye nguvu na taasisi za kifedha za kimataifa wametoa suluhisho za kupunguza mzigo wa madeni kwa Afrika. Kwa sababu mdororo wa kiuchumi unaotokana na janga la Covid-19 unahitaji uwezo mkubwa wa bajeti. Uzito wa madeni ya Afrika huzuia nchi kadhaa kujidhatiti vilivyo kwa kukabiliana na ugonjwa huo.

Kwa kipindi cha miaka kumi, deni la umma kwa Afrika limeongezeka maradufu na kufikia leo dola bilioni 365 ambazo 145 zinadaiwa na China.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anataka Ufaransa na Ulaya kufuta madeni ambayo wanadai Afrika. Lakini hii inhusu tu sehemu ndogo ya mzigo wa madeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.